Header Ads Widget

Mtu mzee zaidi duniani aliyefariki mwaka 2017 akiwa na umri wa miaka 117

 

Emma Morano amefariki akiwa umri wa miaka 117


Mtu mzee zaidi duniani amefariki nchini Italia akiwa na umri wa miaka 117.

Emma Morano alizaliwa tarehe 29 mwezi Novemba mwaka 1899 eneo la Piedmont nchini Italia. Ndiye mtu wa mwisho aliyezaliwa miaka ya 1800 ambaye bado alikuwa hai.

Kuishi kwake miaka mingi kunatajwa kutokana na maumbile ya jeni na chakula chake ambacho ni mayai matatu kwa siku mawili yakiwa ni mabichi.

  • Bi Morano alikuwa kifungua mimba katika familia ya watoto wanane ambao wote washafariki.

Alifariki akiwa nyumbani kwake katika mji wa kaskazini wa Verbania.

Bi Morano akitazama picha yake akiwa mdogo

CHANZO CHA PICHA,EPA

Maelezo ya picha,

Bi Morano akitazama picha yake akiwa mdogo

Alikiri kuwa kuishi kwake kulichangiwa na jeni kwa kuwa mama yake alifariki akiwa na umri wa miaka 91 na dada zeke nao waliishi miaka mingi.

Lakini pia alikuwa akila chakula kisicho cha kaiwada cha mayai matatu, mawili yakiwa mabichi kwa kipindi cha zaidi ya miaka 90.

Daktari wake wa miaka 27 Carlo Bava, aliambia AFP kuwa hakuwa akila mbona wala matunda

Sherehe Bi Morano alipotimzia miaka 117 mwaka uliopita

CHANZO CHA PICHA,REUTERS

Maelezo ya picha,

Sherehe Bi Morano alipotimzia miaka 117 mwaka  mwaka 2017

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI