Header Ads Widget

MKOJANI BALOZI WA KIMOMWE MOTER


Na Fatma Ally MDTV Dar es Salaam

Kampuni ya kimomwe Moters ya uagizaji wa magari kutoka nje ya nchi leo imemtambilisha msanii wa filamu nchini Tanzania maarufu kama Mkojani kuwa  Balozi wa kampuni hiyo 


Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Mkurugenzi na Mwanzilishi wa Kampuni hiyo, Seleman Khalifa Kimomwe, amesema wamekua na uzoefu wa katosha katika uagizaji wa magari. 


"Kampuni yetu imeanzishwa tangu mwaka 2018 mpaka sasa tuna miaka mitatu, tumekua tukiagiza magari kutoka Singapore, Japani na Dubai na wateja wetu wamekua wakifurahia huduma zetu, leo tumemtambulisha Mkojani kwa ajili ya kuitangaza zaidi Kimomwe Moters"amesema Seleman.


Kwa upande wake, Balozi wa kampuni ya uagizaji wa magari kutoka nje Kimomwe Moters, Mkojani amesema kampuni hiyo imekua ya kitofauti kwani mtu anaweza kulipia pesa za gari aliyoagiza kwa awamu mbili na kupata gari lake bila usumbufu.


"Kampuni yetu imekua ya tofauti sana watu wanapoagiza magari kutoka kwetu wanauwezo wa kulipia pesa kwa awamu mbili na kupata gari lake bila usumbufu na hata endapo akishindwa kumaliza pesa akiwa amekwama basi tunaweza kumunganisha na Benki akapata mkopo wa kumalizia gari lake"amesema Mkojani.


Aidha, amesema wateja watakapofika katika kampuni hiyo wataweza kupatiwa washauri na wataalamu wanaojua magari pamoja na mafundi nguli Ili waweze kuchangua magari mazuri na bora.


Ameongeza kuwa, magari watakayoagizwa na wateja yatafika ndani ya siku 45 kutoka siku walizoagiza kutoka nchi yoyote watakayochukua ikiwemo UK, Japan, Dubai pamoja na Singapore.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI