Header Ads Widget

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYOJIRI JANA BUNGENI JIJINI DODOMA

 

Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Ecobank, Bw. Charles Asiedu alipomtembelea leo ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma, Novemba 3, 2021


Katibu wa Bunge, Nenelwa Mwihambi (kulia) katika picha ya pamoja na Katibu wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Raya Msellem alipomtembelea leo ofisini kwake Bungeni 



Wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge (kushoto) wakiwa katika mazungumzo na Wajumbe wa kamati ya Kinga, Fursa na Maadili ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar (kulia) waliowatembelea kwa lengo la kujifunza jinsi kamati hiyo inavyotekeleza majukumu yake kikao kilichofanyika leo katika ofisi za Bunge 


Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge, Emmanuel Mwakilasa (kushoto) akimkabidhi Mwenyekiti wa kamati ya Kinga, Fursa na Maadili ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Panya Abdallah kitabu cha makusanyo ya Sheria mbalimbali zinazotumiwa na Bunge tukio lililofanyika leo katika ofisi za Bunge Jijini Dodoma,


Katibu wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Bi. Raya Msellem akichangia jambo wakati kamati ya Kinga, Fursa na Maadili ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar ilipoitembelea kamati ya kudumu ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka kwa lengo la kujifunza jinsi kamati hiyo inavyotekeleza majukumu yake 

Wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge wakifuatilia mazungumzo na Wajumbe kamati ya Kinga, Fursa na Maadili ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar 


Wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge wakiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa kamati ya Kinga, Fursa na Maadili ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar nje ya jengo la Bunge leo Jijini Dodoma, Novemba 3, 2021

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI