Jeshi la Magereza nchini limepongezwa kwa kubuni utaratibu mzuri wa kujiendesha kimapato kupitia miradi ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa nyumba bora kwa gharama nafuu.
Pongezi hizo zimetolewa mwishoni mwa wiki na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Joseph Mkirikiti wakati alipozindua mradi wa nyumba za kuishi askari na mradi wa maji kwenye gereza la kilimo Mollo wilaya ya Sumbawanga.
Alifurahishwa kuona mradi wa nyumba ya kuishi familia mbili iliyojengwa kwa shilingi Milioni Hamsini na Tano na aliwapongeza kwa kutekeleza dhana ya Magereza Kujitegemea kwa kuwa inaongeza tija kwa mkoa kupitia miradi inayotekelezwa.
“Kama Magereza imeweza kujenga nyumba moja ya familia (Two in One) kwa gharama ya shilingi Milioni 57, huu ni mfano mzuri wa ubunifu. Wito wangu Halmashauri za Rukwa waige mfano huu kwenye utekelezaji miradi ya ujenzi ili kupunguza gharama za fedha za serikali “alisisitiza Mkirikiti.
Awali akitoa taarifa ya miradi, Mkuu wa Gereza la Kilimo Mollo Mrakibu wa Magereza (SP) Nicostratus Magori alisema mradi wa nyumba za kuishi askari umetekelezwa kwa lengo la kupunguza uhaba wa makazi bora ya askari .
Aliongeza kusema gharama halisi za mradi wa nyumba hiyo ni shilingi Milioni 55 ambapo gereza kupitia miradi yake limechangia shilingi Milioni 17.3 na Kamishna Jenerali wa Magereza (CGP) alichangia
Alisema miradi hii licha ya kutuimarisha kiuchumi inasaidia pia kutoa mafunzo ya ujuzi kwa wafungwa ili watakapomaliza vifungo vyao itawasaidia kuwa raia wema kwa kufanya kazi halali
Gereza la kilimo mollo lilianzishwa mwaka 1967 ambapo lina eneo la ekari 8,989 na kwa sasa lina miradi ya ujenzi wa nyumba ya kulala wageni , ujenzi wa bwalo,ujenzi wa fremu 11 za maduka na ujenzi wa viwanda vidogo vya kuchakata mazao ya ngano,alizeti na mahindi
0 Comments