Mwonekano wa machine inayotumika kuandaa juisi ya miwa / picha kutoka mtandaoni.chanzo cha habari hii BMG Online Media |
Ukuaji wa teknolojia hususani mitandao ya kijamii kama vile Facebook, Twitter, Instagram na Whatsupp umesaidia upashanaji taarifa kwa haraka miongoni mwa watumiaji wa mitandao hiyo.
Hata hivyo baadhi ya taarifa ambazo zimekuwa zikichapishwa na watumiaji wa mitandao hiyo zimekuwa zikipokelewa kwa hisia tofauti na hata nyingine kuzua taharuki kutokana na kwamba si taarifa zote zinakuwa za kweli.
Hatua hiyo imesababisha maadhi ya watumiaji wa mitandao ya kijamii kutoamini kwa haraka taarifa wanazokutana nazo kwenye mitandao hiyo hata kama ni za kweli. Hii ni kutokana na taarifa nyingi zinazochapishwa mitandaoni kugubikwa na uzushi mwingi.
Miongoni mwa taarifa iliyochapishwa na mmoja wa watumiaji wa mitandao ya kijamii na kuzua gumzo kwenye majukwaa mbalimbali mitandaoni ni ile iliyoeleza kwamba asilimia kubwa ya juisi ya miwa inayouzwa Nyamagana mkoani Mwanza ina kinyesi.
Taarifa hiyo imechapishwa na mtandaoni na mtu aliyejulikana kwa jina la ‘dr.paulmasua’ ikisomeka “utafiti uliofanywa huko Mwanza na wataalamu kutoka Chuo Kikuu cha Bugando unaonyesha kwamba asilimia kubwa ya juice ya miwa inayouzwa Nyamagana ina mavi.
Utata mtupu
Muda mfupi baada ya taarifa hicho kuchapishwa mtandaoni ilisambaa kwa kasi na kuzua taharuki na mjadala mzito kwenye majukwaa mbalimbali hususani Whatsupp, kila mmoja akitaka kujua ukweli wake.
Baadhi ya wachangiaji walihoji “kwanza Bugando siyo Chuo Kikuu, ni Hospitali ya Kanda hivyo hii taarifa hatuwezi kuiamini”. Pia kutokana na kutoamini taarifa hiyo, wengine walichapisha maoni yenye mzaha yenye kupotosha kama haya “mavi hayana shida kwenye baridi, nitaendelea kuigida kama kawaida kusafisha figo
0 Comments