Header Ads Widget

JESHI LA POLISI TABORA LAFANYA MSAKO NA KUKAMATA BANGI, MALI NA WATUHUMIWA WA UHALIFU.

Jeshi la polisi mkoani Tabora limefanikiwa kukamata madawa ya kulevya aina ya bangi magunia 7 , kifurushi kimoja na debe 1 la Pombe haramu ya Gongo ambavyo ni mazao ya vichocheo vya uharifu. mwandishi wa matukio daima Lucas Raphael anaripoti kutokea Tabora

Akizungumza na waandishi Habari Kamanda wa Polisi Mkoani hapa ACP Richard Abwao katika Kituo cha Polisi mjini Tabora alisema kukamatwa kwa watu  hao kunafuatia kufanyika kwa oparesheni zinazoendelea mkoa hapa .

Alisema kuwa  mnamo Novemba 4 mwaka huu 2021 majira ya saa 1:00 usiku huko kwenye kituo kipya cha mabasi Kata ya Nzega Mashariki Tarafa ya Nyasa Wilaya ya Nzega Mkoani hapa walifanikiwa kumkamata Issa Paul(37) ambaye ni mfanyabiashara na mkazi wa Mkoani Mwanza akiwa na magunia 2 ya bangi na kifurushi kidogo.

Kamanda Abwao alisema kuwa mtuhumiwa alikuwa  akisafirisha kutoka Busondo Wilayani Nzega akipeleka Kirumba Mkoani Mwanza na kwamba mbinu ya kuchanganya mahindi na pumba ilitumika ili kukwepa kubainika ama kuzuia harufu isitoke lakini waliweza kubaini haraka na kumtia nguvuni.

Alisema kuwa mnamo Oktoba 25 mwaka huu 2021 majira ya saa 10:00 usiku huko Mwanasi ndani ya hifadhi ya Igombe Wilayani Uyui Mkoani hapa walifanikiwa kuwakamata watuhumiwa 4 wakiwa na bangi gunia 5 ndani ya nyumba wanayoishi.

“Tulifanikiwa pia kupata bangi mnamo Oktoba 11 mwaka huu 2021 majira ya saa 4:00 usiku huko Mtaa wa Kazima Kata ya Isevya  Manispaa ya Tabora na tulimkamata Filipina Lawama (18) akiwa na debe 1 na hivyo kwa ujumla tumekata magunia 7 na debe 1 na kifurushi kimoja cha bangi”alisema.

Katika tukio lingine Jeshi hilo limefanikiwa kukamata mali zinazoshukiwa kuwa ni za wizi ambapo mnamo Novemba 5 mwaka huu 2021 majira ya saa 9:00 alasiri katika Kata ya Kidongo chekundu Manispaa ya Tabora Mkoani hapa walimkamata mtuhumiwa mwenye umri wa miaka 21 mkazi wa Kata ya Nga’mbo akiwa na radio sabufa 1, spika 2,magodoro 2 , televisheni 1 ndeki 2,mabegi 2,vioo vya magari vya upande,taa 2 za pikipiki,simu,flash,nyundo,bisibisi na funguo mbalimbali.

Kamanda huyo alisema kuwa Novemba mwaka huu 2021 ndani ya Manispaa ya Tabora walifanikiwa kukamata pikipiki aina ya SAN LG yenye namba za usajili MC 537 CQS naa KING LION yenye usajili namba MC 633 CKG na kwamba watuhumiwa wote wanashikiliwa na jeshi la polisi.

“Mnamo Oktoba 29 mwaka huu 2021 Wilayani Uyui katika Kijiji cha Nkulusi Kata ya Ndono Tarafa ya Ilolanguru tulifanikiwa kukamata pikipiki mbili aina ya BOXER na SAN LG kati yake moja ikiwa na namba za usajili MC 713 AXB  na nyingine isiyokuwa na namba”alisema.

Aidha alisema kuwa jumla ya lita 79 za pombe ya moshi walizikamata pamoja mitambo 2 ya kutengeneza pombe hiyo haramu na watuhumiwa 24 walikamatwa kati yao wanawake wakiwa 6 na wote wanashikiliwa na Jeshi hilo na watafikishwa Mahakamani kujibu mashitaka ili sheria ichue mkondo wake dhidi yao.

Alitoa tahadhari kwa wazazi na walezi kuwachunga watoto na vijana wao na kuwafuatilia mienendo yao na kuhakikisha wanawaonya kuacha kujihusisha na vitendo vya kiharifu na makundi yote mabaya na kucha tabia ya kufanya matendo maovu hususani nyakati za mwisho wa mwaka ambapo Jeshi litakuwa makini na kuwakamata wahusika wote.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI