Mkuu wa wilaya ya kibaha Sara Msafiri amefanya ziara ikiwa ni utaratibu wake wa kufanya ziara kwenye kata ambapo ametembelea kata za Pangani na Mkuza na kusikiliza kero za Wananchi na kuzitolea ufumbuzi kupitia mikutano ya hadhara.
Awali alitembelea Daraja la Lumumba linalounganisha Wilaya za Kibaha na Ubungo ambalo limekuwa likilalamikiwa na wananchi kuwa kando ya kutumia gharama kubwa lakini halikamiliki kwa wakati.
Akizungumzia Daraja hilo,Diwani wa kata ya Pangani Mheshimiwa Augustino Mdachi amesema baada ya kuwa kero hiyo iliyodumu kwa muda mrefu mwaka 2016 aliwaandika jeshi la wananchi Tanzania lawaomba daraja la muda na kupewa lililokuwa Mpwapwa lenye uwezo wa kupitisha uzito usiozidi tani 10 na linasafirishwa kwa msaada wa kampuni ya Madalali wa Bima Tanzania kwa kuchangiwa mafuta ya shilingi 15 milioni.
Aidha, Msaada wa kulifunga ulifanywa na Jeshi lenyewe kwa ushirikiano wa Wakala wa barabara za mjini na vijijini TARURA huku wananchi wakichangia chakula cha mafundi eneo la kazi pamoja na vifaa vingine vilivyogharimu 60 millioni Michango ya Wananchi.
Kaimu Meneja wa TARURA Kibaha Donald Mjale amemueleza kuwa katika kukamilisha Daraja serikali kupitia TARURA Imeshatumia milioni 80 kwa kugharamia ununuzi wa kokoto tani 60,waya,bolt nakuchimba mtaro wa kuchepusha njia za maji ili kupunguza hatari ya kuharibu kingo ya Daraja.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kibaha Mhandisi Mshamu Munde amewataka TARURA kuweka jicho la kitalam na ubunifu kwenye Daraja hilo kuwa bado utaalam wao unahitajika ili kuliweka kwenye kiwango bora.
Aidha amewashauri kuweka alama za barabarani ili kutoa tahadhari na kujiridhisha na uzito unaotakiwa kwani kutokana na umri wa vyuma vya daraja hilo kuwa chakavu inashauriwa isizidi tani 5.
Munde amemuomba Diwani wa kata hiyo kufanya ufuatiliaji jeshini kupata taarifa zaidi ya daraja hilo kama limetolewa jumla au limeadhimishwa na iwapo watakuwa wametoa kwa muda basi mamlaka inayohusika iweke mikakati ya kujenga daraja la kudumu siku zijazo.
Mkuu wa Wilaya,Sara Msafiri amewataka viongozi kutoa mrejesho wa mara kwa mara kwa Wananchi juu ya matumizi ya Fedha zao.
Aidha,ametoa rai kwa TARURA,Uongozi wa Kata Na Jeshi kufanya tathimini ya kina ya ujenzi wa Daraja la Lumumba kwa kuanisha kazi zilizofanywa na kutoa ripoti Ofisini kwake ili kujiridhisha na gharama zilizotumika pamoja na kwa mkurugenzi wa Halmashauri.
Mwisho.
0 Comments