Header Ads Widget

DC KARATU: WAKULIMA TUMIENI MBEGU ZA ASILI ZINAVUMILIA UKAME

 



Mkuu wa wilaya ya Karatu Abas Kayanda amesema kuwa kutokana na mabadiliko ya tabia ya nchi yaliyopo hivi sasa wakulima wakitumia  mbegu za asili uwezekano wa kuendendea kuzalisha  ni mkubwa kutokana na mbegu hizo kuvumilia ukame......NA NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA


Kayanda aliyasema hayo wakati akifungua maonesho ya mbegu za asili na vyakula yaliyofanyika Karatu mkoani Arusha ambapo alieleza kuwa wataalamu wameshaeleza kuwa mvua zinazotarajiwa kunyesha ni ndogo na mazao hayo pia yanahitaji mvua kidogo lakini pia mazao hayo ni kilimo hifadhi kwani yanatunza mazingira.


Alieleza kuwa mbegu za asili hazitumii kemikali  lakini pia zina uwezo wa kutumika kwa miaka mingi tofauti na mbegu za kisasa ambazo zinapandwa kwa msimu mmoja na mkulima kulazimika kurudi dukani kununua mbegu nyingine.



Mkuu wa wilaya ya Karatu Mhe. Abas Kayanda akitembelea mabanda pamoja na viongizi wengine


“Tumetembelea mabanda na tumeambiwa kuwa heka moja ya shamba ambalo limepandwa mbegu ya mahindi ya asili inazalisha  karibu gunia 18 jambo ambalo halitofautiani na mbegu za kisasa kwahiyo tunaona mbegu hizi zina faida nyingi sana tofauti na watu wanavyofikiri,”Alisema.


Alifafanua kuwa wilaya ya Karatu ni miongoni  mwa wilaya ambazo zinaongoza kwa kuwa na mbegu nyingi za asili ukilinganisha na maeneo mengine lakini pia inaongoza kwa kuwa na benki za mbegu ambapo kwa msimu ulipita walilima hekari 47,837.5 na kuvuna tani 97,558.9 huku mahitaji yakiwa ni Tani 82,423.8 na ziada kubaki zaidi ya  tani 15,000.

Mbunge viti maalum mwakilishi wa NGO'S Tanzania bara Neema Lugangira.


Mbunge viti maalum mwakilishi wa NGO'S Tanzania bara Neema Lugangira alisema kuwa wataenda kushirikiana na waandaji wa maonesho hayo, serikali pamoja na Bunge juu ya umuhimu wa kuwa na sheria mahususi ambayo inatambua mbegu za asili ili ziweze kutunzwa na kuhifadhiwa,kulindwa usalama wake pamoja kulindwa hati miliki.


Alisema wakulima wengi hawajui mahali pa kuzipata mbegu hizo hivyo kuna haja ya kuwa na benki za mbegu za asili ili waweze kuzipata bila kupitia changamoto  ambapo pia alisema kuwa Kuna changamoto kubwa ya mabadiliko ya tabia ya nchi hali ambayo ipo haja ya kuzitumia mbegu hizo ili kuhifadhia mazingira na kama taifa ni muhimu wazilinde mbegu hizo.



Kwa upande wake Beatus Malema Mratibu wa kilimo ikolojia hai kutoka wizara ya kilimo ambaye pia mkurugenzi msaidizi uendelezaji mazao, pembejeo na ushirika aliwatoa wakulima wasisi kuhusiana na changamo zinazowakabili ikiwemo kutokutambulika kwa mbegu na kusema kuwa serikali inazitambua mbegu hizo na haidharau ndio maana kuna tasisi za serikali kama vile TARI wanaoshughulika na mbegu hizo.


“Niwaambie tuu kuwa changamoto zote mlizozitoa hapa nazichukua na tutaenda kuzifanya kazi kwasababu tunadhamini jambo kubwa kama hili na hatujazisahau kama watu wanavyosema kwani imeshakubalika kuunda kitengo kitakachishulika na kilimo cha ikolojia na niwaahidi kuwa tutawaelimisha wataalamu wetu ili kuweza kuimarisha eneo hili,” Alisema.



Naye mchungaji John Safari mwenyekiti wa mtandao wa vikundi vya wakulima Mkoa wa Arusha (MVIWAARUSHA) alieleza kuwa mradi wa kilimo endelevu unatekelezwa kwa miaka mitano wilayani Karatu ambapo lengo la maonesho hayo ni kujenga uelewa kwa jamii juu ya mfumo wa mbegu zinazosimamiwa na wakulima juu ya uzalishaji wa kiikolojia na mfumo endelevu wa chakula.


Alisema pia wana lengo la kujenga na kuimarisha uhusiano wa wakulima na wadau wengine wanaotoa huduma za kilimo ambapo kauli mbiu ya maonesho hayo kwa mwaka huu“MBEGU ZA ASILI KWA MIFUMO ENDELEVU YA CHAKULA” ambapo mfumo huo ukifanikiwa utaleta uhuru wa mbegu za wakulima  pamoja na kuwashawishi watunga sera na serikali kuzitambua mbegu.

Mkuu wa wilaya ya Karatu Abas Kayanda akitembelea mabanda pamoja na viongizi wengine

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI