Mwenyekiti wa Taifa wa CUF Prof Lipumba (Picha ya maktaba )
Na Fatma Ally MDTV Dar es Salaam
Chama Cha wananchi (CUF) kimewavua uanachama, wanachama saba wa chama hicho, na wengine kupewa onyo na karipio kali huku wakitakiwa kukata rufaa ndani ya siku 14 endapo watahisi wameonewa.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Afisa Mawasiliano kwa umma wa chama hicho, Eng Mohamed Ngulangwa kwa niaba ya Mwenyekyeti Prof Harouna Lipumba amesema kuwa, maamuzi hayo yametolewa na baraza Kuu la uongozi la Taifa baada ya kufanyika kikao Nov 5-6 mwaka huu kilichokaliwa na wajumbe wa baraza hilo.
Amesema kwa, mujibu wa Katiba ya chama hicho, Toleo la mwaka 2019 ibara 10 (1)(c) inawapa haki wale wote wanaojihisi kutotendewa haki katika maamuzi ya kinidhamu yaliofanywa na baraza kuu la uongozi la Taifa kukata rufaa mkutano mkuu wa Taifa ndani ya siku 14 tangu maamuzi wanayoyapinga kutolewa.
Aidha, amewataja waliovuliwa uanachama huo, ni pamoja na Hamida Abdalla, Dhifaa Mohamed Bakari,Mtumwa Ambar Abdallah, Chande Jidawi, Ali Makame Issa, Mohamed Vuai Makame pamoja Abdul Juma kambaya aliyekua Mkurugenzi wa kitengo Cha habari na mawasiliano wa chama hicho.
Katika hatua nyengine, baraza hilo, limempitisha Mbarouk Seif Salim kuwa Mjumbe wa baraza kuu aliyeteuliwa na Mwenyekiti wa chama Taifa,kwa mujibu wa ibara za 81(2) na 94(1)(I) za Katiba ya chama ya 1992, toleo 2019, pia limemchagua mjumbe huyo kuwa Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, kwa mujibu 98 (1) ya Katiba ya chama 1992 toleo la 2019.
Hata hivyo, baraza hilo limewapitisha Rajab Mbarouk 'Ranz' kuwa Katibu wa kamati ya itifaki na udhibiti kwa mujibu wa ibara ya 91(1) na Mwadini Jecha aliyeteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Mipango na uchaguzi.
"Viongozi hawa wote waliopitishwa na baraza kuu la uongozi la Taifa baada ya kuteuliwa na Mwenyekiti wa chama Taifa Prof Haruna Lipumba, wamejaza nafasi zilizokuwa wazi baada ya viongozi waliokuepo awali uteuzi wao kutemguliwa"amesema Eng Ngulangwa.
Hata hivyo, baraza hilo, limetoa onyo kwa maandishi kwa kuzingatia ibara ya 83(5)(a) ya Katiba ya chama ya mwaka 1992, toleo 2019 kwa Mussa Haji Kombo, Yasin Mrotwa, Ali Rashid Abarani, Said Omari huku ikitoa kario Kali kwa Hamid Bobali na Masoud Ali Said.
Aidha, amempongeza Rais wa JMT Samia Suluhu Hassan kwa hotuba nzuri aliyoitoa huko Scotland kuhusu mabadiliko ya tabia nchi, huku wakitoa wito kwa Rais Samia juu ya ujenzi wa demokrasia imara nchini Tanzania na kuona umuhimu wa kutimiza azma yake ya kukutana na viongozi wa vyama vya siasa nchini kwa mustakali wa amani utulivu na utawala bora nchini.
0 Comments