Mkuu wa wilaya ya Siha Thomas Apson
Na Rehema Abraham Kilimanjaro
Serikali mkoani Kilimanjaro, imeipongeza benki ya ushirika Kilimanjaro KCBL kwa kuweza kuwanyanyua wakulima wa zao la kimkakati la kahawa kwa kuwakopesha pembejeo za kilimo na ufugaji.
Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Mkuu wa wilaya ya Siha Thomas Apson , ameyasema hayo Novemba 10,2021 mwaka huu mjini Moshi wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa Huduma Mbadala na za Kidigitali za benki ya KCBL zilizofanyika katika makutano ya barabara ya posta mkoani hapa.
Apson amepongeza benki ya kcbl kwa kuwawezesha wananchi wenye mitaji kidogo kuweza kukopa na kuweza kuendesha shughuli zao jambo ambalo limewezesha benki hiyo kutengeneza faida ya shilingi milioni 20 katika robo ya tatu ya mwaka huu.
Aidha mkuu huyo ameipongeza KCBL kwa kuja na mpango wa huduma Mbadala na za Kidigitali za benki hiyo ambapo wananchi walioko kwenye vikundi wataweza kunufaika na mikopo yenye riba nafuu.
Awali akizungumza Mwenyekiti wa bodi ya benki ya ushirika Kilimanjaro KCBL Dkt. Gervas Machimu amesema wakati wanaanza benki hiyo ilikuwa na hasara ya shilingi milioni 600, ndani ya robo ya tatu za mwaka huu wametoka kwenye hasara hiyo na kupata faida takribani shilingi milioni 20.
"Tulianza benki hii ikiwa na hasara ya kiasi cha shilingi milioni 600, ndani ya robo ya tatu ya mwaka tumetika kwenye hasara tumefidia na Sasa tuna faida ya shilingi milioni 20,"amesema Dkt. Machimu.
Dkt. Machimu amesema wakati huo watu walikuwa hawawezi kuchukua fedha zao ewalizokuwa wameziweka kwenye benki kama amana, lakini tuwahudimia wote hao.
Kwa upande wake meneja Mkuu wa benki ya ushirika Kilimanjaro KCBL Godfrey Ng'urah, amesema kuwa kwa sasa mteja mwenye kadi ya Visa card ya benki ya ushirika kcbl anauwezo wa kutumia kwenye ATM za benki ya CRDB, lakini pia na kwa mawakala wa benki ya CRDB.
0 Comments