Header Ads Widget

AKUTWA AMEUWAWA MACHO YATOBOLEWA

Kijana ambaye hajafahamika jina wala makazi yake, anayekadiliwa kuwa na umri wa miaka (25-30), amekutwa ameuawa na kutobolewa macho katika Ghuba la kuhifadhia uchafu la Ngokolo mitumbani Manispaa ya Shinyanga. mwandishi wa matukio daima Mapuli Misalaba anaripoti kutokea Shinyanga

Mwenyekiti wa mtaa wa Mwinamila katika eneo hilo la tukio Amir Athumani, alisema tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo ambapo amesema baada ya kufika eneo la tukio majira ya saa moja asubuhi, aliukuta mwili wa kijana huyo akiwa ameuawa kinyama na kutobolewa macho, na watu ambao bado hawajafahamika.

" Tukio hili ni la pili la watu kuuawa kwenye Ghuba hili la uchafu, akiwamo na mtoto mdogo kuuawa na kuweka ndani ya boksi, hivyo naomba wananchi kama wana migogoro, watafute ufumbuzi na kuacha kujichukulia sheria mkononi," alisema Athumani.

Aidha Athumani alisema  watu mbalimbali wamefika kuuona mwili wa kijana huyo, lakini hakuna ambaye amemtambua, ambapo bado wanaendelea na jitihada na kutambua ndugu zake, ili wapatikane na kuupunzisha  mwili kwenye makazi yake ya milele.

Kwa upande wake Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga Kamishna msaidizi wa Polisi George Kyando, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo, na kubainisha bado wanafanya upelelezi ili kubaini wauaji pamoja na chanzo chake.

Kamanda Kyando alisema katika eneo la tukio, Jeshi la Polisi walikuta pembeni ya mwili wa marehemu kuna vyuma, ambavyo wanazani ndivyo vimetumika kufanyia mauaji, na kueleza kuwa Mwili wa marehemu umehifadhiwa kwenye chumba cha maiti katika Hospitali ya Rufani mkoani Shinyanga.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI