Header Ads Widget

IRINGA INAHITAJI TAA ZA KUONGOZA MAGARI (TRAFIKI LIGHT )SALIM ASAS


Mwenyekiti wa kamati ya usalama barabarani mkoa wa Iringa Salim Asas amewaomba wakala wa barabara TANROAD kuweka taa za kuongozea magari barabarani maharufu kama trafic light ili kupunguza msongamano wa magari pamoja na wananchi kwa wakati mmoja .
Diana Bisangao wa matukio daima

Aliyasema hayo alipokuwa akizungumza na wafanyakazi wa sekta mbalimbali pamoja na wananchi katika uzinduzi wa wiki ya nenda kwa usalama iliyofanyika leo Oktoba 9 katika viwanja vya stendi ya zamani vilivyoko Iringa Mjini.

Asas ambae pia ni Mjumbe wa NEC Taifa  alisema kuwa kumekuwa na magari mengi pamoja na wananchi katika matumizi ya barabara hivyo  kusababisha msongamano mkubwa mjini kitu ambacho kinaweza kupelekea ajali.

''katika manispaa yetu ya Iringa kumekuwa na msongamano mkubwa wa magari, ukizingatia barabara yetu ya kuelekea Dodoma imekuwa na idadi kubwa ya magari makubwa na watumiaji ni wengi sana hii barabara hivyo tunaomba watu wa tanroad kutuwekea taa za kuongozea magari ili zitusaidie katika kujua nani anatakiwa apite na nani asipite kwa wakati huo'' alisema 

Kwa upande wake Kamanda wa Jeshi la Polisi kitengo cha usalama barabarani mkoa wa Iringa RTO Yusuph Kamotta alisema kuwa wamefanya uzinduzi huo kwa lengo la kupambana na ajali za usalama barabarani kwa kutoa elimu na kukagua vyombo vya moto na kusema vipo vyanzo vitatu vya ajali za barabarani ambavyo ni makosa ya kibinadamu hii ni asilimia 76, ubovu wa vyombo asilimia 16 na miundo mbinu asilimia 8.


'' sisi kama jeshi kuanzia trafiki makao makuu, ngazi ya mkoa na ngazi ya wilaya tuna utaratibu wa kutoa elimu, kwahiyo hii elimu kwetu ni endelevu na katika wiki hii tutaongeza spidi ya kutoa elimu kukabiliana na usalama wa barabarani, tunakagua vyombo kwa sababu ni chanzo kimojawapo cha ajali, na asilimia kubwa imechukuliwa na makosa ya kibinadamu kama uendeshaji wa mwendokasi, ulevi, uchovu, ugonjwa  na msongo wa mawazo''.

Hata hivyo kamanda alisema kuwa dereva peke yake anachangia ajali kwa asilimia 72 hivyo wabadirike ili kupunguza hizo ajali na kipindi hiki endapo dereva atakamatwa kwa kosa la kusababisha ajali hatolipa faini bali atapelekwa katika vyombo vya sheria na kufungwa.

Hata hivyo alitoa wito kwa madereva na watumiaji wa barabara kubadirika na kutoa ushirikiano kwa vikosi vya usalama na pia kwa abiria kutoa taarifa kwa polisi wa barabarani pindi wanapoona dereva anaendesha vibaya usafiri walioupanda.




   

Post a Comment

1 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS