Klabu ya Yanga SC Kibabe imekataa kudanganywa na Ice cream za Azam kuwa wao Si watoto hivyo kuamua kuigagadua kama si kuifunga basi kuichapa goli 2-0 na hivyo kufanikiwa kupata ushindi kwenye mchezo wake wa nne wa Ligi Kuu ya NBC .
Katika mchezo huo uliopigwa kwenye uwanja wa Benjamini Mkapa Jijini Dar es Salaam. Magoli ya Yanga katika mchezo huo yamefungwa na Fiston Mayele dakika ya 36′ pamoja na Jesus Moloko dakika ya 73′. Yanga imeanza ligi vizuri ambapo mechi zote nne imefanikiwa kupata ushindi na sasa ndio inaongoza ligi ikiwa na alama 12, wakifunga mabao 6 huku wakiwa hawajaruhusu bao hata moja. Mechi inayofata Yanga itakuwa tena katika uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam, Novemba 2, 2021 kuvaana na Ruvu Shooting
0 Comments