Naibu Waziri wa Kilimo nchini Mh. Hussein Bashe amesema kuwa Wizara ya kilimo itaanzisha kitengo maalum ndani ya Wizara kitakachohusika na masuala ya kilimo hai ili kukuza na kuendeleza kilimo hicho hapa nchini. MWAMDISHI Rehema Abraham ,MDTV Dodoma.
Aidha Wizara kwa kushirikiana na Wadau wa kilimo nchini, wataanzisha pia benki ya Mbegu kwa lengo la kuendelea kuhifadhi mbegu mbalimbali za asili zitakazomsaidia mkulima kutekeleza kilimo hai chenye tija hapa nchini.
Akiwa mgeni rasmi katika kongamano la kilimo hai lililowakutanisha wadau wa kilimo kutoka maeneo mbalimbali lililofanyika mjini dodoma waziri Bashe amesema kuwa Wizara itaanzisha benki ya Mbegu kwa lengo la kuendelea kuhifadhi mbegu za asili zitakazomsaidia mkulima kutekeleza kilimo hai .
Katika hatua nyingine amesema kuwa kuna baadhi ya maduka yanauza mbegu za kisasa (high breed) lakini huwezi kukuta duka linauza mbengu za asili kwa sababu hazipatokani, hivyo amesema ili viweze kupatikana kwa wingi ni lazima zizalishwe kwa wingi.
"Sisi kama wizara katika nchi hii ni lazima tuanze mchakato wa kuanzisha benki kubwa ambayo itakuwa kwa ajili ya kusafisha mbegu,kuzalisha mbegu za asili ili ziweze kupatikana kwa wingi kwa ajili ya wakulima wetu ,"amesema Bashe.
Kwa upande wake mwenyekiti wa Tasisi ya kuendeleza kilimo hai Tanzania Dr.Mantima Juma (TOAM ) amesema kuwa afya zimekuwa zikibadilika sana kutokana na mfumo wa uzalishaji wa vyakula ambao umeharibubika .
Amesema kuwa katika suala la viatilifu ni vyema kuepuka kununua na wakulima wakatengeneza wenyewe ili kupunguza uharibifu wa mazingira ambao umekuwa ikitokea.
"Kwa hiyo suala Zima tunalolijadili hapa ni suala mtambuka na katika siku mbili hizi tutatazama nyanja zote kwa mtazamo mmoja ,niikisema kilimo hai sio mazao peke ake tu bali ni pamoja na mifugo kwa hiyo ni mjadala mpana sana ambao tutaweza kujadili katika kilimo "Alisema





0 Comments