Wanawake katika Kijiji cha Isanzu Kata ya Manda Wilayani Songwe Mkoani Songwe wamesema kuwa wanalazimika kujifungulia vichakani au kwa waganga wa kienyeji kwa kile wanachodai kukwepa manyanyaso kutoka kwa muuguzi wa zahanati ya Kijiji hicho.
Hayo yamebainishwa katika mkutano wa kijiji ambapo wananchi walihoji kuhusu hatua zilizochukuliwa kutokana na wananchi kulalamika muda mrefu kuhusu mwenendo wa muuguzi aliyetajwa kwa jina la Mary Yohana kuwanyanyasa wanawake na watu wanaoenda kupata huduma kwa kuwatolea lugha za kuudhi sambamba na kuwafukuza pindi wanapohoji taratibu za malipo ya huduma katika zahanati hiyo.
Baada ya mwandishi wetu kumtafuta muuguzi huyo ili kutaka kujua ukweli wa madai ya wananchi hao.muuguzi alieleza kuwa hawezi kueleza chochote mpaka apewe ridhaa ya kuzungumza sakata Hilo namwajiri wake ambaye ni Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri hiyo.
Baada ya jitihada hizo Mwandishi wetu alimtafuta mganga mkuu wa wilaya ya Songwe Humphlay Masuki ambaye alidai swala Hilo limefika ofisini kwake na wameshafanya hatua za kumwamisha kituo muuguzi huyo hivyo ndani ya wiki moja atakuwa ameondoka katika Kijiji hicho.
Mwisho.
0 Comments