Header Ads Widget

WANANCHI WATAKIWA KUSHIRIKI SHUGHULI ZA UJENZI WA MADARASA


Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Diwani wa kata ya Ndala iliyopo Manispaa ya Shinyanga Zamda Shabani amewataka wananchi wa kata hiyo kushiriki kikamilifu katika shughuli ya ujenzi wa vyumba vya madarasa yanayojengwa shule ya sekondari 

Ametoa wito huo leo wakati wa shughuli ya kuchimba msingi kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa viwili na ofisi katika shule hiyo ambapo kata hiyo imepatiwa fedha kiasi cha shilingi milioni 40 na serikali ili kutekeleza ujenzi huo.


“Lazima kila mwananchi aweze kushiriki katika zoezi hili la maendeleo kwa sababu maendeleo haya siyo ya mtu mmoja kwahiyo kila mwananchi lazima ahamasike kuunga juhudi hizi ili na yeye achangie upande wa maendeleo” amesema 


Kwa upande wake Mtendaji wa kata hiyo Lukas Magandula amesema kuwa shule hiyo inaupungufu  wa vyumba vya madarasa vitano ambapo wameanza ujenzi wa  vyumba viwili  hivyo wamejiwekea mikakati ya kuhakikisha mwaka kesho changamoto hiyo inatatulika.

Aidha Magadula amewaomba wananchi kuendelea kushiriki kwenye shughuli hiyo ili kukamilisha ujenzi huo kwa muda sahihi

“Lakini pia kunawananchi ambao hawajafika siku ya leo bado tunakazi nyingi za kufanya kwa sababu maelekezo ni kwamba nguvu kazi ya ujenzi inatoka kwa wananchi bado kunakazi ya kusogeza matofali, kusogeza kokoto na shughuli zingine”

Akizungumza  makamu mkuu wa shule hiyo Alphonce Dea amesema shule hiyi inaidadi ya wanafunzi zaidi ya 450 ambapo vyumba vya madarasa ni saba huku wakitegemea kupata wanafunzi wengene wanao anza kidato cha kwanza mwaka kesho 



Dea amesema changamoto ya vyumba vya madarasa ikitatulike shule hiyo itafanya vizuri zaidi darasani kitaaluma kwani mwalimu atakuwa na uwezo wa kumfikia mwanafunzi mmoja mmoja 

“Ni dhahiri tukiwa na vyumba vya kutosha tutafanya vizuri zaidi darasani kuliko mwalimu kushindwa kufika kwa wanafunzi kwa sababu ya idadi kubwa ya wanafunzi darasani tunaiomba serikali iendelee kuwa na jitihada za kuhakikisha tunapata vyumba vya wanafunzi iwapo vyumba hivi vikikamilika taaluma yetu itaimarika zaidi”

 Wananchi wa kata hiyo wameishukuru serikali kwa kuwapatia fedha kiasi cha  shilingi milioni 40 kwa ajili ya kuongeza madarasa katika kata yao.

Shughuli ya kuchimba msingi kwa ajili ya kujenga vyumba vya madarasa mawili na ofisi moja imeanza leo kata ya Ndala ambapo viongozi mbalimbali wa chama wameshiriki katika shughuli hiyo.




Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI