Katika Mkutano huo kwa pamoja wamekubaliana kushirikiana katika mapambano dhidi ya magonjwa mbalimbali ikiwemo ugonjwa wa UVIKO-19 ili kulinda afya za wananchi wa Tanzania na Uganda.
Aidha, Dkt. Gwajima amemhakikishia utayari wa Wizara yake kushirikiana na Wizara yake nchini Uganda ili kuboresha utoaji huduma kwa wananchi na kuleta matokeo chanya katika Sekta ya Afya baina ya nchi hizo.
Naye Waziri wa Sayansi, Teknlojia na Ubunifu nchini Uganda Dkt. Monica Musenero amesema, Uganda iko tayari kushirikiana na Tanzania katika mapambano dhidi ya magonjwa mbalimbali ikiwemo ugonjwa wa UVIKO-19.
Kikao hicho kimefanyika katika kituo cha mikutano ya kimataifa cha Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.
0 Comments