Header Ads Widget

WANANCHI WA BUHIGWE WAFURAHIA KUSOGEZEWA CHANJO YA UVIKO-19.


WANANCHI katika Wilaya ya Buhigwe Mkoani Kigoma wamefurahia kusogezwa kwa huduma ya chanjo uviko…19 kupitia mikusanyiko mbalimbali hiyo imewapunguzia adha ya kutembelea umbali mrefu kufuata huduma hiyo.Mwandishi wa MDTV  Editha Karlo,anaripoti toka Buhigwe

Wakiongea kwenye mkutano wa kutoa elimu ya chanjo na kuhamasisha kuchanja zoezi lilikuwa likifanywa na waandishi wa habari kwa kushirikiana na timu ya afya ya Wilaya ya Buhigwe katika soko la Buhigwe baadhi ya wananchi wamefurahi zoezi hilo na kuipongeza serikali kwa uamuzi huo mzuri.


"Tumefurahi kusogezewa huduma hii ya chanjo awali umbali wa kufuata chanjo na kukosa elimu ili kuwa sababu ya wengi kushindwa kuchanja lakini sasa hivi mambo ni mazuri kama hivi mmetufuata hapa sokoni kutupa elimu na kutuchanja hapa hapa"alisema Martha Chiguti mfanyabiashara katika soko la Buhigwe

Mwandishi wa habari wa star TV mkoa wa Kigoma Richard Katunka akiwaelewaza wananchi wa buhigwe umuhimu wa chanjo ya uviko…19 ,kwenye viwanja vya soko la Buhigwe

Ibrahimu Ndameze mkazi wa Buhigwe mfanyabiashara katika soko la Buhigwe anasema alikuwa ana subiria kwa hamu kupata elimu ya chanjo hiyo sambamba na kuchanja pamoja na kupewa cheti sababu yeye ni mfanyabiashara huwa ana safiri mara kwa mara kupata cheti cha chanjo kutamuondolea usumbufu wakati wa safari zake.


"Yaani nilipoliona tu gari la afya hapa sokoni nimefunga biashara yangu kwa muda kuja kusikiliza elimu hii ya chanjo ya uviko…19,nina washukuru nawashauri ambao hawajapata chanjo hii wasisite,binafsi sijaona kama kuna shida yoyote tujitokeze kwa wingi kupata chanjo hii wataalamu wetu wa afya wanapopita"alisema


Naye mwandishi wa habari wa star tv Mkoa wa Kigoma Richard Katunka alisema  alisema kuwa uamuzi wa kutoa elimu ya chanjo ya uviko…19 na kuhamasisha wananchi wanafanya kwa lengo la kuhamasisha jamii kuondokana na dhana potofu ya kwamba chanjo hizo si salama.


Katunka alisema kuwa chanjo ya uviko…19 siyo lazima inatolewa kwa hiyari lakini wananchi wanatolewa shaka na waendelee kupata chanjo kwakuwa haina madhara yoyote na inasaidia kutokupata maambukizi kwa kiwango kikubwa.


"Niwaombe ndugu zangu tupate chanjo hii kwani ni salama na watafiti wamethibitisha hili pamoja na shirika la afya ulimwenguni,sasa hivi tuna vuta hewa ya Mungu bure hatulipii,ila ukiumwa corona hewa utailipia kwa kununua mtungi wa gesi kila baada ya masaa ili kunusuru uhai wako,wangapi wanaweza mudu hizo gharama?ujanja ni kuchanja ndugu zangu"alisema Katunka


Baadhi wananchi wanaofanya biashara katika soko la Buhigwe wakiwasikiliza wahamasishaji wa chanjo ya uviko19(hawapo pichani)wakati wakiwapa elimu ya chanjo


Naye mratibu wa chanjo wa Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe Stephano Joseph Mabula alisema huduma hiyo sasa inatolewa katika vituo vyote vya afya lakini pia,lakini pia wanatoa huduma hiyo kwa njia ya mkoba unaotembea ambapo  huwafuata wananchi katika kaya kwa kaya na  maeneo ya shughuli zao ili waweze kuwafikia wananchi wanahitaji chanjo.

Mwisho

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI