Header Ads Widget

WAKAZI WA DODOMA KUTUMIA KIPIMO CHA JIPIME

Wakazi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma wametakiwa kujitokeza na kutumia kipimo cha JIPIME ili kupima hali ya maambukizi ya virusi vya UKIMWI. mwandishi wa matukio daima Dennis Gondwe anaripoti kutokea Dodoma.

Kauli hiyo ilitolewa na Afisa Muuguzi wa Zahanati ya Makole, Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Lilian Baliza alipokuwa akitoa elimu ya kutumia kipimo cha JIPIME kwa ajili ya kupima hali ya maambukizi ya VVU katika banda la Afya la Jiji la Dodoma lililopo Bustani ya Mapumziko Chinangali jijini Dodoma kwenye maonesho ya Karibu Dodoma Festival.

Baliza alisema “sisi Idara ya Afya tupo hapa kwa lengo la kuelimisha watu kupima wenyewe kwa kutumia kipimo cha JIPIME baada ya kuwapa elimu ya namna ya kujipima. Sababu kubwa ya kufanya hivyo ni imani tuliyonayo kuwa siyo watu wote wana uwezo wa kwenda kwenye vituo vya kutolea huduma za afya. Hivyo, tunatoa elimu ya umuhimu wa kujua hali ya maambukizi na kupelea elimu hiyo kwa wenza na watu wengine ili nao waweze kuchukua hatua ya kujipima”.

Alisema kuwa mtu akiwa na maambukizi anapewa rufaa kwenda katika kituo cha kutolea huduma za afya, ushauri na tiba ya VVU.

Aidha, aliwashauri wananchi kwenda kupata elimu ya huduma ya JIPIME kwa kutumia kipimo binafsi ya VVU. “Athari za mtu kutofahamu hali yake ya maambukizi ya VVU ni kubwa. Moja ni kuambukiza wengine ambao hawana maambukizi” alisema Baliza.

 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI