Header Ads Widget

VISA VYA UKATILI WA KIJINSIA VYABAINIKA JIJINI MWANZA

 



Na Adrian Audax - MDTV Mwanza


Mkuu wa kituo cha Nyakato, Dastun Kombe ametoa taarifa ya uwepo wa vitendo vya ukatili katika maeneo mbalimbali ya jiji la Mwanza,


Taarifa hiyo imewasilishwa katika kikao maalum cha halmashauri ya Chama Cha Mapinduzi ambacho kimehudhuriwa na wajumbe wa kamati ya siasa, wajumbe halmashauri kuu, wenyeviti wa mtaa, watendaji wa vijiji, wakuu wa shule za msingi na sekondari, Jopo la wataalamu, Madawati ya kijinsia pamoja na Jeshi la polisi



Kombe amesema kuwa ndani ya siku tatu watoto watatu wenye umri chini ya miaka minne wamefanyiwa matukio ya kikatili katika kata ya Mahina na Mhandu, huku akieleza kuwa watoto hao walichukuliwa kwa madai ya kwamba wanaenda kununuliwa pipi lakini kwa hali isiyo ya kawaida hufanyiwa vitendo vya ubakaji na watu hao,


Pia ameongeza kuwa kuna tukio lilifanyika maeneo ya Shibula ambapo mtoto mwenye umri wa miaka 2 na mwezi 1 alibakwa, Pia katika Iyabo mtoto wenye umri wa miaka 3 na mwingne mwenye umri wa miaka 4 walifanyia ukatili huo. Watoto wote wamefikishwa katika vituo vya afya na matibabu yanaendelea


Mkuu wa upelelezi wilaya ya Nyamagana Ins R. Mapungu  amesema kuwa Jeshi la polisi tayari limeanza msako wa kuwabaini wahalifu katika mitaa yote na zoezi hilo linafanyika pia kupitia mikutano ya hadhara inayoandaliwa na serikali ya kata,


Naye Mbunge wa Jimbo la Nyamagana Mhe. Stansilaus Mabula ameonesha kusikitishwa na taarifa hizo za kikatili na kuwataka wazazi pamoja na walezi wa watoto kutoa ushirikiano kwa Jeshi la polisi ili kubaini wahalifu hao na kuwachukulia hatua za kisheria,



Akitoa ushauri kwa wazazi ili kuepusha mazingira ya vitendo hivyo  Mstahiki Meya wa halmashauri ya Jiji la Mwanza Sima Costantine amewataka wazazi kuwajengea watoto wao mazingira ya kutozurura  hovyo pia   amewataka wenyeviti wa vitongoji kuandaa mikutano kwa kushirikiana na Jeshi la polisi ili kutoa elimu juu ya ulinzi wa watoto,


MWISHO

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI