Na Rehema Abraham MDTV Kilimanjaro
Wanachi mkoani Kilimanjaro wametakiwa kunywa kwa wingi maziwa kwani Yana faida nyingi kwenye mwili kwani imeonekana kuwa unywaji wa maziwa upo chini ukilinganisha na nchi jirani ya Kenya na ugaanda.
Amesema hayo mchungaji mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania KKKT Kennedy Kisanga wakati akiwa katika maenesho ya siku ya chakula duniani yanayoendea katika viwanja vya Mandela vilivyopo pasua mkoani Kilimanjaro.
Aidha amsema kuwa wamekuwa wakisisitiza wanafunzi mashuleni kunywa maziwa kwani wanapokunywa maziwa inaboresha Afya kutokana na kuwa na virutubisho vyote ambayo yanahitajika kwenye mwili wa binadamu.
"Tumesema tuanze na watoto ili kuwapandikizia hamu ya kunywa maziwa maana vinginevyo watoto watavutwa kunywa soda na vinywaji vingine venye sukari "Alisema Kisanga.
Sambamba na hayo amesema kuwa ni vyema mwanadamu aknywa Lita arobaini za maziwa kwa mwaka kwani anapaswa kunywa asubuhi jioni na pale anapomaliza mlo wake .
Amesema kuwa kipindi Cha nyuma wazazi walikuwa wakijifungua chakula chao kikuu kilikiwa maziwa lakini kwa wakati huu wamekuwa hawatumii kwa vile watu hawapo Tena kwenye upatikanaji wa maziwa ,kwani kipindi Cha nyuma Kila mchaga alikuwa anafuga.
Hata hivyo amesema mkoa wa Kilimanjaro umetajwa kuwa na kwashakoo ambapo ametaja sababu ni kitokunywa maziwa .
Akiwa katika maonesho hayo katibu wa Wizara ya Mifugo na uvuvi, Rashid Tamatama, amesema kuwa ulaji wa nyama na unywaji wa maziwa nchini bado uko chini na imekuwa changamoto kubwa kwa mujibu wa Shirika la Chakula la Umoja wa Mataifa (WFP).





0 Comments