SIHA
Mapema leo Oct 10 majira ya saa 1:00 asubuhi katika mashamba ya Nafco kijiji cha Ngarenairobi wilaya ya Siha mnyama aina ya twiga amekufa baada ya kupigwa na umeme akitokea kwenye ushoroba wa hifadhi ya mlima Kilimanjaro
Kamanda wa polisi mkoa wa Kilimanjaro ACP Simon Maigwa amesema kutokana uhaba wa maji wanyama wamekuwa wakihama kutoka eneo moja kwenda lingine kutafuta maji na ndivyo kama huyu twiga alivyokatiza kwenye nyaya za umeme na kusababisha kifo chake na kuwa kipindi hiki cha kiangazi wananchi wachukue tahadhari
Wakati huo huo mtuhumiwa mmoja anayehisiwa kuwa na ugonjwa wa akili katika eneo la Samana kijiji cha Mese wilaya ya Siha amemuua kwa kumkata na kitu chenye ncha kali mtoto Johson Ronald Munuo(6)na kisha kuua ndama kwa kutenganisha kichwa
Kamanda Maigwa amesema mbinu aliyotumia nikuchukua panga linalotumika kukatia majani ya ng'ombe na akiwa kwenye banda la ng'ombe alimkata ndama shingoni nakufa kisha kuelekea alipokuwa mke wa mtuhumiwa akinywa chai na kutekeleza mauaji ya mtoto huyo
.





0 Comments