Kaimu Mkurugenzi wa Tari kituo cha Tumbi Dr Emmanuel Mrema amesema kuwa watanzania wanapaswa kutumia mchicha lishe kwa wingi zaidi ili kuboresha afya zao. mwandishi wa matukio daima anaripoti kutoka Tabora
Kauli hiyo ameitoa wakati alipotembelewa waandishi wa habari ofisini kwake ambapo alisema kuwa mchicha ulikuwa unachukuliwa kwa wepesi zao la kawaida ambalo halipewi nafasi.
Alisema kuwa kwa sasa tunahamasisha watu kutumia mchicha kwa wingi ambao tunaamini kuwa mtuamiaji anaweza kupata madini.
“Huu mchicha una viini lishe vingi na madini ambayo huwezi kuzipata kwenye vyakula vingine ni vema watu wakawa nao kwenye bustani za nyumbani ili kuboresha afya zao” alisema Dr Mrema
Nae Mtafiti wa Kituo cha Utafiti Tari Tumbi Tabora Matha Ndelemba alisema kuwa mchicha lishe unavirutubisho vingi tofauti na mchicha mwingine ambao tunatumia majumbani.
“Mchicha tumeanza kuungiza katika kituo cha Fatuma Mwasa Ipuli kwa uzalishaji wa mbegu ili kuzisambaza nchini katika maeneo mbalimbali, lakini upo utofuati unaweza kupata vitu vingi ambavyo unaweza kuchanganya uji, keki, chapati juice vyote vinatokana na mchicha lishe ambavyo vinafaida kubwa” alisema Ndelemba
0 Comments