Header Ads Widget

SHINDANO LA KUMTAFUTA TANZANIA TOP MODEL 2021/2022 LAJA KIVINGINE

 



Na Mwandishi Wetu.


MKURUGENZI  wa kampuni ya mavazi ya paka wear fashion, Bw. Gymkhana Majaliwa ametambulisha rasmi kuendeleza na kuandaa shindano la la Mwanamitindo bora wa mfano wa Tanzania 2021/2022 (Tanzania top model ) ambalo kwa mwaka huu linakuja kivingine.


Akizungumza na waandishi wa habari, Gymkhana ameshukuru wadau mbalimbali ambapo ameahidi kuendeleza makubwa ya sindano hilo ambalo awali lilikuwa likiendeshwa na Tanzania Top Role model Agency Limited chini ya Bw. Jackson Kalikumtima.


Gymkhana amesema wamekuja na mpango mkakati ya kulifanya shindano hilo kuwa zaidi ya  kawaida kwa kufungua fursa mbalimbali zilizopo duniani na kuzileta katika jamii ya Kitanzania.


"Tanzania top model msimu wa 2021/2022 itarushwa katika kipindi cha luninga (Reality televisheni show) kwa muda wa miezi mitatu na Watanzania watapata fursa ya kuwaona na kuwapigia kura ilikupatikana mshindi." Alisema Gymkhana. 


Kwa upande wake Meneja miradi wa kampuni ya Paka Wear, Bw. Adili Kigoda alisema shindano hilo litaendeshwa katika kanda teule mbalimbali ikiwemo Tanzania Bara na Zanzibar. 


"kauli mbiu yetu ni 'Uanamitindo wenye malengo" hivyo mshindi ataingia mkataba na Kampuni yetu kwa muda wa mwaka mmoja na nusu kwa lengo la kufanya kazi za sanaa ya mavazi na kijamii.


Aidha, zawadi kwa washindi ni pamoja na mshindi wa kwanza pesa taslimu Tsh milioni 5, mshindi wa pili na wa tatu kila mmoja atazawadiwa  Milioni 2 na mshindi wa Wanne hadi wa 10 watazawadiwa cheti cha ushiriki.


Kwa upande wake Afisa sanaa kutoka Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA), Selemani Kharifa Mabisso alisema kama Serikali watahakikisha wanasimamia maadili na kuendeleza utamaduni wa mtanzania kwa nyanja mbalimbali ikiwemo mitindo na ubunifu.


Nae Mwanaharusi Mwilima wa  udada club ambaye pia ni Mkurugenzi wa kampuni ya Jollie pad ambao ni wadhamini wa onesho hilo alisema  wamejipanga kuhakikisha binti wa kike anaonesha umodel wake pasipo mashaka na kuzingatia maadili ya Mtanzania. 


Kwa upande wake, mkufunzi na Mkurugenzi wa kampuni ya La Vitoiro, Bi. Mary Chizi alisema watahakikisha wanazingatia vigezo vya ushiriki kwa wasichana wote watakaobahatika msimu huu.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI