Header Ads Widget

RAIS WA ZANZIBAR MHE.DK.HUSSEIN ALI MWINYI AZURU KABURI LA MAREHEMU JOHN POMBE MAGUFULI NA ATEMBELEA MAONESHO YA WIKI YA VIJANA NA

 

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge, Uratibu Kazi Ajira Vijana na Wenye Ulemavu Mhe Jenista Joakim Mhagama,wakimsikiliza Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Kanda Chato Dr.Marygoreth  Changaluda alipotembelea alipotembelea mabanda ya Maonesho ya Wiki ya Vijana yanayofanyika katika viwanja vya Mazaina Chato.(Picha na Ikulu)


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi wakimsikiliza Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Zanzibar Ndg. Yussuf Juma akitowa maelezo ya bidhaa mbalimbali zinazotengenezwa na Mabaraza ya Vijana Zanzibar, wakati alipotembelea banda lao katika maonesho ya Wiki ya Vijana yaliofanyika katika viwanja vya Mazaina Chato Mkoani Geita.(Picha na Ikulu)



WANANCHI wa Chato Mkoani Geita wakishangilia wakati Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayuko pichani) akiwahutubia katika viwanja vya Mazaina Chato baada ya kutembelea Maonesho ya Wiki ya Vijana yaliofanyika katika viwanja hivyo.ikiwa ni shamrashamra za Kilele cha Mbio za Mwenye wa Uhuru na Kumbukizi wa Kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. (Picha na Ikulu)




WASANII wa Kikundi cha Taraab cha Wajelajela wakitowa burudani katika viwanja vya Mazaina Chato wakati wa maonesho ya Wiki ya Vijana yaliofanyika katika viwanja hivyo.(Picha na Ikulu)


WANANCHI wa Chato Mkoani Geita wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) akiwahutubia katika viwanja vya mazaina Chato, baada ya kutembelea Maonesho ya Wiki ya Vijana yaliofanyika katika viwanja hivyo.(Picha na Ikulu)


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwahutubia Wananchi wa Chato Mkoani Geita katika viwanja vya Mazaina, baada ya kutembelea maonesho ya Wiki ya Vijana yaliofanyika katika viwanja  hivyo.(Picha na Ikulu)


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiweka shada la maua katika kaburi la aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Marehemu John Pombe Magufuli, alipofika nyumbani kwa marehemu kusalimia familia ya marehemu Chato na (kushoto) Mjane wa Marehemu Mama Janeth Magufuli na Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi.(Picha na Ikulu)

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akitowa salamu za heshima baada ya kuweka shada la maua katika kaburi la aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Marehemu John Pombe Magufuli alipofika nyumbani kwa marehemu Chato kusalimia familia ya marehemu na (kushoto) Mjane wa Marehemu Mama Janeth Magufuli na Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi.(Picha na Ikulu)


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Mjane wa Marehemu Mama Janeth Magufuli (kulia kwa Rais) Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said, baada ya kumaliza kuweka maua katika kaburi la Marehemu John Pombe Magufuli nyumbani kwa marehemu Chato Mkoani Geita.(Picha na Ikulu) 



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI