SERIKALI imeendelea kuboresha Sekta ya Teknolojia ya Habari na mawasiliano (TEHAMA) ndani ya nchi Kwa kufunga mkongo ya mawasiliano nchi mbalibali pamoja na kuondoa Kodi kwenye Vifaa vya TEHAMA .Mwandishi wa Matukio Daima Media anaripoti
Akitoa taarifa ya wiki ya Serikali mbele ya wanahabari leo mkoani Iringa Kuelekea miaka 60 ya Uhuru wa Tanganyika ,msemaji mkuu wa Serikali Geryson Msigwa alisema serikali imepiga hatua kubwa Katika maendeleo mbali mbali yakiwemo ya TEHAMA .
Alisema Katika kuhakikisha TEHAMA inakuwa nchini Serikali imeamua kuondoa Kodi hiyo ili kukuza sekta ya mawasiliano nchini na Kila mmoja aweze kunufaika na mawasiliano .
Alisema Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan imedhamilia kuendelea kukuza huduma za mawasiliano Kwa njia ya kidgitali Hali itakayopelekea uchumi wa nchi kukuwa na wananchi kuondokana na kadhia ya mawasiliano kama ilivyokuwa miaka ya nyuma .
Msigwa alisema kumekuwepo na maendeleo makubwa ya Teknolojia ya Habari na mawasiliano nchini na Rais Samia ameendelea kuwekeza nguvu Katika sekta hiyo hasa ukizingatia kuwa Dunia ya Sasa ni ya kiutandawazi zaidi na uchumi umekuwa ukikua Kwa kutegemea utandawazi .
Alisema Kwa ajili ya kuboresha Sekta ya mawasiliano Serikali iliamua kuongeza bajeti Kwa wizara husika kutoka shilingi bilioni 11 Hadi kiasi cha shilingi bilioni 241 Kwa ajili ya kuboresha zaidi sekta hiyo na sio kwenda kulipana Posho .
,,sehemu kubwa ya Fedha hizi zitakwenda Katika ujenzi wa mkonge wa mawasiliano wa Taifa pia kama alivyosema mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kuwa Tanzania inakwenda kujenga chuo kikubwa Afrika Mashariki na Kati cha mawasiliano ili vijana wakasome wapate ujuzi na kazi hiyo itakamilika wakati wowote,,
Pia alisema kuanzia kesho jumatatu Mawaziri wataanza kukutana na wanahabari jijini Dodoma Kwa Kila Waziri kueleza kwenye sekta yake ni mafanikio gani yamepatikana ili kabla ya siku ya kumbukumbu ya miaka 60 ya Uhuru watanzania wajue Kazi na maendeleo yaliyofikiwa kwenye wizara mbali mbali .
Akielezea Kuhusu mradi wa kuendeleza maliasili na kukuza utalii mikoa ya nyanda za juu kusini (REGROW)alisema kuwa mradi huo ni mkubwa na ikumbukwe Taifa linategemea utalii Kwa asilimia 17.2 hivyo kupitia mradi huo uchumi wa nchi utaendelea kukua za
Alisema utalii unazalisha ajira Milioni 1.6 nchini hivyo sekta hiyo ni nyeti japo ilikuwa ikikua mikoa ya kaskazin pekee .
Alisema mradi wa REGROW utatumia zaidi ya shilingi Milioni 345 kuhakikisha unakuza utalii mikoa ya nyanda za juu kusini .
0 Comments