Na Adrian Audax - MWANZA
Jimbo la Nyamagana linatarajia kupokea mgao wa fedha za Kitanzania Bilioni Moja kwa ajili ya Ujenzi wa Vyumba vya madarasa pamoja na kuweka madawati,
Hayo yamebainishwa na Mbunge wa Jimbo la Nyamagana Mhe Stansilaus Mabula alipokuwa akizungumza na Wajumbe wa halmashauri ya Chama cha Mapinduzi katika kata ya Mkolani wilani Nyamagana,
Mhe Mabula amesema kuwa fedha hizo zitasaidia kupunguza uhaba wa vyumba vya Madarasa pamoja na Madawati ambayo takribani vyumba vya Madarasa 98 vitajengwa pamoja na madawati yake,
Fedha hizo zimetolewa kutoka halmashauri ya Jiji la Mwanza kupitia mpango wa Ustawi wa Taifa na mapambano dhidi ya Uviko19 uliozinduliwa October 10 na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan wenye malengo ya kuinua uchumi,
Sambamba na hayo Mgao huo umefanyika latika halimashauri zingine za Mkoa wa Mwanza ambapo halimashauri ya Manispaa ya ilemela itajengwa vyumba vya madarasa 97, Buchosa 128, Kwimba 109, Magu 123, Misungwi 146, Sengerema 129, na Ukerewe 155 hivyo kukamilisha idadi ya vyumba vya madarasa 985 ambavyo vinapungua katika halimashauri zote Jijini Mwanza





0 Comments