Shirika lisilo na kiserikali la mtandao wa watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI(NACOPHA) kupitia mradi wa hebu tuyajenge umekabidhi pikipiki mbili Katika Halmashauri za wilaya ya Iringa .
Meneja wa mradi huo Kanda ya Mbeya Frednand Mazuni alisema kuwa pikipiki hizo pia zimetolewa kwenye Halmashauri 15 nchini zinazotekeleza mradi huo .
Alisema kuwa pikipiki hizo zitasaidia watenda kazi kufuatilia mwenendo wa mradi huo .
"Kwa mwitikio wa mapambano ya UVICO 19 shirika hili limekabidhi Vifaa mbali mbali vya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona Kwa watu wenye maambukizi ya virusi vya UKIMWI "
Mwenyekiti wa Umoja wa watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI (KONGA) Halmashauri ya Iringa Justin Mfilinge akishukuru Kwa msaada huo alisema kuwa vitendea kazi hivyo ni hatua kubwa ya Utekelezaji wa shughuli zao za Kila siku .
Alisema kabla ya kupewa pikipiki walikuwa wakitumia gharama zao kufuatilia taarifa kwenye kata ila Sasa wataepuka gharama hizo.
Kwa mratibu wa UKIMWI na tiba Katika Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Godfrey Mtunzi alisema kuwa kuwa msaada huo umekuja wakati husika na kuwa itasaidia Katika mapambano dhidi ya UVICO 19 .
Alisema vitakasa mikono vilivyotolewa pamoja na barakoa vitasaidia Katika mapambano ya UVICO 19 Katika Halmashauri ya Manispaa ya Iringa hasa maeneo ya kwenye kata .
Kaimu mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Omary Mkangama amepongeza jitihada hizo za wadau hao Katika mapambano dhidi ya UVICO 19 Katika Halmashauri hiyo .
Alisema Halmashauri ya Manispaa ya Iringa imeendelea na mapambano ya UVICO 19 Kwa kuchukua tahadhari zote zinazotolewa na wataalam wa afya na kutaka wananchi kuendelea kuchukua tahadhari pamoja na kupata Chanjo ya UVICO 19
0 Comments