CHAMA cha Mapinduzi CCM Kimekipongeza chama cha ACT Wazalendo kwa kushinda jimbo la konde liliopo mkoa wa kaskasini Pemba Wilaya ya Micheweni .Na Hamida Ramadhan MDTV Dodoma
Akiongea leo jijini Dodoma Katibu NEC Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka amesema hiyo ndio demokrasia kama ambavyo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Samia Suluhu Hassan alivyo ahidi mara baada ya kuapishwa kuwa Rais kwamba kwenye uongozi wake ataimarisha dhana nzima ya siasa safi na demokrasia ndani ya nchi yetu.
"Kwahiyo tunawapongeza wenzetu wa chama cha ACT wazalendo kwa kushinda jimbo hilo la konde mkoa wa Kaskazini Pemba Wilaya ya micheweni hongera kwao," amesema Shaka
Pia amesema wanawashukuru wananchi na wanachama wa Jimbo la Konde kwa kukichagua Chama cha Mapinduzi ijapokuwa kura hazikutosha tunaendelea kuwashukuru kwa kujitokeza na kupiga kura .
"Ni ukweli kwamba zile kura ambazo amepata mgombea wa CCM sisi tunaamini ndizo alizopata lakini pia tukumbuke usemi wa wahenga ya kwamba kuvunjika kwa koleo sio mwisho wa uhunzi tutaendelea kujipanga na kushiriki kwenye chaguzi zinazofuata," Amesema Shaka.
Aidha amesema kumalizika kwa chaguzi hizo ndogo kwa upande wa CCM Jimbo la Ushetu ilishinda 96.6 na kwa jimbo la konde Mgombea Mohamed Said Issa Wa chama cha ACT Wazalendo ametangazwa kuwa mshindi kwa kupata Kura 3408 .
Hata hivyo kwa upande wa mgombea wa CCM Mbarouk Amour Habibu alipata kura 794 kati ya kura 3388 zilizopigwa.
Aidha amesema ushindi wa jimbo la konde ni kama funzo kubwa kwani watanzania tunaweza kufanya siasa na kuuwisha na kutukuza demokrasia yetu na ikawa funzo kwa wengine wanaoiangalia Tanzania kama Kioo katika mfumo wa vyama vingi.
Mwisho..
0 Comments