Na, Titus Mwombeki-BUKOBA.
Mkuu wa mkoa wa Kagera Meja Jenerali Charles Mbuge ameagiza TANROAD inayoshughulika na uratibu wa ujenzi wa daraja la Kitengule lililopo Wilaya ya Misenyi mkoani humo lililoghalimu jumla ya Bil. 25.4 kuakikisha linakamilika ndani ya wiki sita ili kuwezesha uvunaji wa miwa, kuongeza uzalishaji wa sukari na kuepusha serikali kukosa mapato.
Ameyasema hayo alipotembelea mradi huo akiambatana na viongozi mbalimbali wa mkoa huo ili kujionea ujenzi wa wa daraja hilo ulipofikia ambapo amesema serikali inayoongozwa na Rais Samia Suruhu Hassan inania njema ya kuakikisha wawekezaji waliowekeza katika nchi ya Tanzania wanafanya kazi zao katika mazingira mazuri ilikuweza kupata kodi ya ukuwrzesha serikari kuendesha shughuli zake na kuzalisha ajira nchini.
“Serikali inayongozwa na rais Samia Suruhu Hassan inania njema ya kuakikisha wawekezaji katika nchi yetu wanafanya shughuli zao katika mazingira mazuri ili waweze kutoa kodi na kuendelea kuzalisha ajira nchini, hivyo basi nataka ndani ya wiki sita daraja hili liwe limekamilika ili kuwawezesha wawekezaji wa kiwanda cha kagera sukari kufanya shughuli zao”. Amesema Mbuge.
Aidha, mkuu wa mkoa huyo ametembelea mradi wa ujenzi wa bomba la kusukuma maji linalotegemewa kumalizika ndani miezi sita lenye uwezo wakusukuma maji 25 mita kyubiki kwa lisaa linalojengwa na kiwanda cha kagera sukari linalo ategemewa kuongeza uzalishaji kutoka tani laki moja na elfu sabini,pia ameridhishwa na kasi ya ujenzi wa mradi huo nakuwasihi wafanyakazi wa bomba hilo kuendelea kuchapa kazi nakuawambia ofisi yake hiko wazi endapo kutakuwepo na changamoto yoyote wasisite kuwasiliana naye.
Naye afisa zalishaji wa kiwanda cha Kagera Sukari Vicent Mtaki amesema kuwa kutokana na kuchelewa kwa ujenzi wa daraja la Kitengule ambalo lilitegemewa kukamilika mwezi wa saba mwaka huu utapelekea kiwanda hicho kushindwa kuongeza uzalishaji.
“Kutokamilika kwa daraja hili kutapelekea kiwanda kushindwa kuongeza uzalishaji, mpaka sasa kuna tani laki moja na thelasini elfu zilizotegemewa kuvunwa mwezi wa nanne na watisa katika eneo hili lakini zimekwana kuvunwa kutokana na kutokamilika kwa daraja hili, kwa hali hii tutashindwa kukuza na kuongeza naksi katika nchi yetu na miwa hiyo itaaribika na kupelekea kiwanda chetu na nchi kupata hasara kubwa ya Bil.36, hivyo tunaomba daraja hili likamilike kwa kipindi kisichozidi wiki sita kwani kutofanya hivyo kutapelekea kuingia katika kipindi cha mvua na sisi kushindwa kuvuna miwa hii yote".
Kwaupande wa Eng. Ntuli kaimu Meneja waTANROAD Kagera ambao niwatekelezaji wa ujenzi wa daraja hilo wamesema wamesema kuwa ujenzi wa daraja hilo ulikwama kutokana na vyuma kukwama bandarini na mpaka Sasa ujenzi umefikia 69.01%.
“Ujenzi wa daraja hili ulianza tarehe 26 Octoba 2018 na ulitegemewa kumalizika tarehe 9 Desemba 2021 lakini ujenzi ulikwama kutokana na vyuma kukwama bandalini suala lilipelekea ujenzi kukwama lakini mpaka sasa ujenzi wa daraja hili umefikia 69.01% na tunaahidi hadi kufikia tarehe 15 ya mwezi Novemba mwaka huu ujenzi wa daraja utakuwa umekamilika”





1 Comments
Kazi iendelee 🔥🔥🔥🔥
ReplyDelete