Header Ads Widget

MKUU KKKT DKT SHOO ATAKA DAYOSISI YA MAANDALIO MAFINGA WASONGE MBELE

 


MKUU wa kanisa la kiinjili la kilutheri Tanzania (KKKT)Dkt Frederick  Shoo asema ameona  kazi kubwa zinazofanywa na kanisa hilo dayosisi ya maandalio ya Mafinga na kuwataka kuendelea na kazi ya Mungu wasirudi nyuma  .

Kauli ya Dkt Shoo imekuja huku kukiwa na sintofahamu kwa waumini wa kanisa hilo jimbo la Mafinga ambao walitengwa na dayosisi ya kusini kwa zaidi ya miaka minne sasa.

Dkt Shoo ametoa Kauli hiyo leo wakati wa ibada maalum ya changizo la ujenzi wa kanisa la Usharika wa Kinyanambo Mafinga wilaya ya Mufindi mkoani Iringa .

Amesema kazi inayofanywa kwenye kanisa hilo ni kubwa na inaonekana na kuwa wasikubali kurudi nyuma wala kukatishwa tamaa  na mtu katika kuifanya kazi hiyo ya Mungu .


Dkt Shoo alisema jitihada zinazofanywa kwenye kanisa hilo dayosisi ya maandalio  ni kubwa na kuwa ameambiwa kuwa eneo hilo linajengwa kanisa la Ghorofa na kuna jingine limekamilika tena la Ghorofa. 

"Niseme tu kazi inayofanywa ni kubwa sana katika eneo hilo na inaonekana pia nikupongeze sana askofu mstaafu wa KKKT dayosisi ya Iringa  Dkt Owdenburg Mdegella  kweli unafanya kazi kubwa sana kusimamia dayosisi hii ya maandalio kweli wahenga walisema nyani Mzee amekwenda mishare mingi nakupongeza " alisema Dkt shoo 

Alisema kuwa kuna dhawabu kubwa kumtumikia Mungu japo wapo watu wanaamini kuwa wapo kwa ajili ya kumtumikia Mungu kwa faida  .

"Futeni hayo mafundisho yanasema tumika ili ubariki bali toa kwa sababu na toa kwa kuwa "

Alisema wale wanaoingia kwa Nguvu zao badala ya kuponya wamekuwa wakizalisha machungu  kwenye nafasi zao .




Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI