Header Ads Widget

MKOA WA PWANI KUANZISHA MAENEO YA VIWANDA.


MKOA wa Pwani unatarajia kuanzisha maeneo maalumu ya Viwanda (Industrial Park) kwenye Halmashauri zote 9 za mkoa huo ili kurahisisha masuala ya uwekezaji.


Hayo yamesemwa mjini Kibaha mkuu wa mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge alipofanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) Dk James Mataragio.


Kunenge amesema kuwa amekutana na viongozi wa Shirika hilo kwa lengo likiwa kuwaeleza mipango ya Uwekezaji ya Mkoa huo na   kupata Mipango Shirika la TPDC ya Usambazaji wa Gesi kwenye maeneo ya Uwekezaji.


"Mkoa unaenda kufanya Uzinduzi wa mpango wa Uwekezaji wa Viwanda (Industrial Mapping) tutawashirikisha TPDC kwenye uzinduzi huo na  vikao vya mabaraza ya Biashara ya Wilaya ambapo wawekezaji wengi wamemweleza kuwa changamoto yao kubwa ni upatikanaji wa Umeme wa Uhakika na Gesi,"alisema Kunenge.


Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa (TPBC) Dk James Mataragio amesema kuwa wameunganishia viwanda  katika Wilaya ya Mkuranga ambapo viwanda vitano na wametumia takribani Bilioni 15 na kwa sasa mradi wa kuleta gesi hiyo Kibaha na Chalinze kwa kujenga kituo eneo la Viwanda Zegereni.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI