Na Hamida Ramadhan ,Dodoma
MFUMUKO wa bei wa Taifa kwa mwaka ulioishia Septemba 2021 umeongezeka hadi asilimia 4.0 kutoka 3.8 kwa mwaka ulioishia mwezi Agosti 2021.
Akiongea na waandishi wa Habari leo Mkurugenzi wa Sensa za watu na Takwimu za Jamii Ofisi ya Taifa ya Takwimu Ruth Minja amesema hilo ni badiliko la asilimia 0.2 ikilinganishwa na nchi jirani kama Kenya na Uganda ambapo septemba 2021 umeongezeka kwa asilimia 0.3 kwa kila moja kukiwa na maana kuwa kuongezeka huko kunaashiria kasi ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia septemba 2021 imeongezeka ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo agosti mwaka huu.
Amesema kuongezeka kwa mfumuko wa bei kwa mwaka ulioishia Septemba 2021 kumechangiwa na kuongezeka kwa mfumuko wa bei wa baadhi ya bidhaa za vyakula na bidhaa zisizo za vyakula kwa Mwezi Septemba, 2021 ikilinganishwa na mwezi Septemba 2020
"Kwa baadhi ya bidhaa za vyakula zilizo changia kuongezeka kwa mfumuko wa bei ni pamoja na unga wa ngano 6.8, nyama ya ng’ombe3.4, maziwa
ya unga 9.2, mayai 5.0 na viazi mviringo 4.7 ," amesema Minja
Kwa upande mwengine amesema baadhi ya bidhaa za vyakula zilizochangia kuongezeka kwa mfu.uko wa bei nipamoja na gesi ya kupikia kwa asilimi 2.7 mkaa kwa asilimia 3.5 na
huduma ya malazi kwenye nyumba za kulala wageni kwa asilimia 5.7.
Hata hivyo amesema mfumuko wa bei wa taifa kwa mwezi septemba 2021 wa
asilimia 4.0 bado upo ndani ya lengo la serikali la muda mfupi na wa
kati wa kuwa na mfumuko wa asilimia 5 ambao unawezesha shughuli za
kiuchumi kufanyika bila athari, na kwamba serikali inaendelea kufanyia
kazi changamoto zinazofanyia bei na huduma kupanda.
Kwa upande wa nchini Kenya mfumuko wa bei umeongezeka hadi asilimia 6.91kwa mwaka ulioishia mwezi Septemba 2021 kutoka asilimia 6.57 kwa mwezi agosti 2021 huku nchi ya
Uganda ukiongezeka hadi asilimia 2.2 kutoka asilimia 1.9.





0 Comments