Serikali imesema Kati ya mikoa inayofanya vizuri Katika kuchangia Pato la Taifa ni pamoja na Mkoa wa Mwanza ikitanguliwa na Jiji la Dar es salaam. mwandishi wa matukio daima Chausiku Said akiripoti kutokea Mwanza
Kwa Mujibu Wa Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msingwa, kutokana na Mkoa huu kuwa nafasi ya pili kiuchumi Serikali inatupia jicho la kutosha kwa kutambua ukubwa na mchango wake kwa Taifa.
Akitoa taarifa ya Wiki Jijini Hapa Msigwa ameeleza kuwa yapo mambo mengi yanayofanywa na serikali katika Mkoa wa Mwanza tangu kuanza kwa Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan.
Ameeleza kuwa katika kipindi cha miezi sita Serikali imetoa kiasi cha Shilingi Billion 344 Mkoani Mwanza kwaajili ya kutekeleza miradi mbali mbali ya wananchi ikiwepo ujenzi wa masoko, stendi kubwa za mabasi na usafili wa majini.
"Ili kuendelea kuinua pato la Taifa kwa Mkoa wa Mwanza tayari tumeleta Shilingi Billion 219.1 kwa ajili ya kutekeleza miradi ya ujenzi peke yake" alisema Msigwa.
Ameitaja miradi hiyo kua ni pamoja na stendi za Nyamhongolo (79%) na Nyegezi (zimeletwa Shilingi Billion 14.2) ambapo kwa ujumla itagharimu kiasi Cha Shilingi Billion 44.7.
Miradi mingine ni ujenzi wa soko la kisasa la katikati ya mji wa Mwanza litakalojengwa kwa gharama ya shilingi Billion 8 na mpaka sasa mradi umefikia asilimia 42% ya ujenzi na kwamba utakapo kamilika utagharimu kiasi cha shilingi Billion 20.3.
Ujenzi wa jengo la abiria kwenye uwanja wa ndege Mwanza kwa Shilingi Billion 13.3, ujenzi wa Mv. Mwanza kwa Shilingi Billion 89.154, ujenzi wa Daraja la Kigongo-Busisi kwa Shilingi Billion 699.278.





0 Comments