Diwani wa kata ya Kibeta wilaya ya Bukoba mkoani Kagera Anastela Buchwa ameishukuru serikali kwa kutoa Milioni 20 mpaka sasa kwaajiri ya ujenzi wa zahanati katika kata hiyo ili kuwanusuru wananchi ambao walikuwa wakifuata huduma za afya kwa mwendo mrefuNa, Mwandishi Titus Mwombeki anaripoti kutoka Bukoba
Ameyasema hayo leo wakati akishirikiana na wananchi wa kata hiyo katika shughuli za kuandaa eneo ambalo limetengwa kwa ajiri ya ujenzi wa zahanati hiyo, amesema kuwa serikali ilitenga mil.50 kwaajiri ya ujenzi wa zahanati katika kata hiyo hivyo mpaka sasa tayari kwenye akaunti ishawekwa mil.20 kwaajiri ya kuanza kazi ya ujenzi wa Zahanati hiyo itakayojengwa katika mtaa wa Omukibeta.
“ Baada ya kupata kiwanja tulienda kwa Mkurugenzi ilikuomba hela za ujenzi wa Zahanati, na Mkurugenzi alikuja na kukagua eneo hilo na kuridhika ndipo aliposema tusubiri wafanye utaratibu wa kupata hela za ujenzi na baadae niliitwa na kuambiwa tutapewa mil.50 na mpaka sasa tumewekewa mil.20 kwenye akaunti ndio maana leo tumeanza maandalizi ya kufanya usafi katika eneo hii kwaajiri ya ujenzi Zahanati hii”.
Sambamba na hilo, In wananchi wa kata hiyo kushirikiana na viongozi wao katika ujenzi wa Zahanati hiyo kwani nguvu yao inahitajika sana ili kufanikisha ujenzi wa Zahanati hiyo unaotegemewa kuanza wiki kesho.
Aidha, Idrisa Rashid mkazi wa Kata ya Kibeta amesema kuwa ujenzi wa Zahanati kwao kama wananchi wameripokea kwa furaha kubwa kwani nimuda murefu wananchi wa kata hiyo wamekoswa sehemu ya karibu yakutibiwa.
“Mimi kama mkazi wa kata ya kibeta nimepokea jambo hili kwa furaha kwani tangu muda mrefu tumekuwa tukiangaika hasa akina mama pamoja na wazee kufuata matibabu kwa mwendo mrefu, kwahiyo ujenzi wa Zahanati katika kata yetu ni Baraka kwetu”.
Bi. Elizabeth Byarugaba mwenye umri wa miaka 75 na mkazi wa kata hiyo ambaye pia ameshiriki katika shughuli ya kufanya usafi katika eneo ambalo Zahanati itajengwa amesema anaishukuru serikali kwa kusilikiliza kilio chao, wazee wa kata hiyo wamekuwa wakiangaika sana hasa katika kupata huduma za kiafya kutokana na ukosefu wa kituo cha afya katika kata yao.
“Tunaishukuru serikari kwa kutukumbuka hasa katika suala la ujenzi wa kituo cha afya kwani tumekuwa tukiangaika sana hasa wazee kufuata huduma za afya mbali kutokana na ukosefu wa kituo cha afya kilicho karibu na hii ni kama neema na baraka kutoka kwa Mungu”.
0 Comments