Header Ads Widget

MBUNGE PROF. NDAKIDEMI AWAASA WANANCHI KUJITOKEZA KWA WINGI KUMSIKILIZA RAIS SAMIA KESHO. .

 


Na WILLIUM PAUL, MOSHI. 

MBUNGE wa Jimbo la Moshi vijijini, mkoani Kilimanjaro  Prof.  Patrick Ndakidemi amewaomba wananchi wa jimbo hilo kujitokeza kwa wingi kesho katika eneo la daraja la Rau kumlaki na kumsikiliza Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassani. 


Prof. Ndakidemi amesema kuwa Rais atafika katika daraja hilo kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa daraja hilo ambalo ni kiunganishi kikubwa kwa wananchi wa Jimbo la Moshi vijijini na Moshi mjini. 


Alisema kuwa, awali kukatika kwa daraja hilo kuliosababishwa na mvua zilizonyesha kulisababisha kero na hadha kubwa kwa wananchi ambapo kilio hicho kilimfikia Rais Samia na kuamua kutoa fedha za ujenzi wa daraja jipya na kesho anaweka jiwe la msingi.


Mbunge huyo alidai kuwa,  mara baada ya kuweka jiwe la msingi atazungumza na wananchi watakaokuwa eneo hilo na badae kuelekea katika viwanja vya chuo kikuu cha ushirika kuzungumza na wananchi.


"Wananchi tujitokezeni kwa wingi katika daraja la Rau na badae viwanja vya chuo kikuu cha ushirika Moshi kumsikiliza mama yetu Rais Samia Suluhu Hassani ujumbe ambao ametuletea wananchi wa Jimbo la Moshi vijijini na mkoa Kwanzaa ujumla" alisema Prof. Ndakidemi. 


Ikumbukwe kuwa, Rais Samia Suluhu Hassani atawasili mkoani Kilimanjaro leo kwa ziara ya siku mbili ambapo kesho anatarajiwa kufungua barabara ya Sanya juu wilayani Siha, kuweka jiwe la msingi katika jengo la mama na mtoto katika hospitali ya rufaa ya mkoa Mawenzi,  jiwe la msingi katika Daraja la Rau na badae kuongea na wananchi uwanja wa Ushirika. 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI