Header Ads Widget

MAUAJI YA SIR DAVID AMESS YALIKUWA UGAIDI

Mauaji ya mbunge wa chama cha conservative nchini uingereza Sir David yanachukuliwa kama kitendo cha ugaidi. Sir David Amess alichomwa kisu katika eneo la bunge lake huko Essex siku ya Ijumaa.

Polisi walisema kuna uwezekano wa tukio hilo kuhusishwa na msimamo mkali wa Kiislam.

Hata hivyo walisema mwanamume mwenye umri wa miaka 25 alikamatwa kwa tuhuma za mauaji baada ya shambulio hilo katika kanisa huko Leigh-on-Sea.

Kama sehemu ya uchunguzi, maaafisa wanapekua maeneo mawili ya makazi mjini London, polisi ilisema.

Maafisa wanaamini mwanamume huyo alitekeleza mauaji hayo peke yake lakini uchunguzi kuhusiana na tukio hilo unaendelea. Manamume huyo anazuiliwa mjini Essex, polisi iliongeza.

Vyanzo vya serikali vimeiambia BBC kuwa ni raia wa Uingereza, kutokana na uchunguzi wa awali, anaonekana kuwa wa asili ya Somali.

Sir David, 69, ambaye alikuwa anawakilisha bunge la Southend West, alikuwa akikutana na watu wa eneo lake -ambapo wapiga kura wanakutana na mbunge na kujadili masuala yanayohitaji kushughulikiwa - katika kanisa la Belfairs Methodist siku ya Ijumaa wakati aliposhambuliwa.

Mkuu wa Polisi wa Essex Konstebo BJ Harrington alisema Sir David alikuwa "akitekeleza majukumu yake wakati maisha yake yalipokatizwa vibaya".

Polisi wa kukabiliana na ugaidi wanashirikiana na polisi wa Essex na kitengo cha eneo la mashariki cha oparesheni maalum.

"Tukio la Leigh-on-Sea limetajwa kuwa kitendo cha ugaidi, na uchunguzi unaongozwa na polisi wa kukabiliana na ugaidi,"  Polisi ilisema.

"Uchunguzi wa awali umebaini kuwa motisha inayoweza kuhusishwa na msimamo mkali wa Kidini."

Maafisa wanaomba kwa mtu yeyote aliye na habari yoyote au na picha kutoka kwa kamera ya CCTV, au video ya kengele ya mlango kuwasiliana nao.

Chanzo; BBC Swahili

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI