Shambulizi hilo limefanya jumla ya vifo vilivyo ripotiwa na maafisa wa afya kutokana na mfululizo wa mashambulizi ya mabomu ya ndege toka wiki iliyopita kufikia 12 na majeruhi 55.
Jeshi la Ethiopia, lilitoa taarifa ikieleza kwamba shambulizi la sasa lililenga kiwanda cha Mesfin, ambacho kinaelezwa kilikuwa cha matengenezo ya vifaa vya jeshi kilichokuwa kikitumiwa na kundi la TPLF.
Lakini mashuhuda walisema kuwa shambulizi hilo la majira ya asubuhi lililenga eneo la makazi ya watu.
Walioshambuliwa walikimbizwa hospitali ya rufaa ya Ayder, ambapo mmoja wa majeruhi alisema kwamba bomu lilishambulia nyumba yake.
Chanzo; VOA Swahili
0 Comments