Happines Laiza mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Mafinga
Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Mji Mafinga limempongeza mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Happines Laizer Kwa kusimamia vizuri Halmashauri hiyo na kupelekea kuongoza Katika mtihani wa Utamilifu ulioiwezesha Halmashauri hiyo kuongoza Kwa mkoa wa Iringa.
Pongezi hizo zimetolewa Leo Katika Kikao cha baraza la Madiwani lililofanyika Leo kwenye Ukumbi wa Halmashauri hiyo.
Akitoa pongezi hizo kwenya baraza Kwa niaba ya baraza mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Reginald Kivinge alisema pamoja na pongezi za Madiwani Kwa wataalam ila kazi hiyo imesimamiwa na mkurugenzi wa Halmashauri hiyo hivyo anastahili pongezi nyingi .
Katika hatua nyingine baraza limempongeza Halmashauri Kwa kutenga Fedha kiasi cha shilingi Milioni 98 Kwa ajili ya ununuzi wa eneo la shule ya Nyamalala ili kupunguza msongamo wa wanafunzi.
Alisema shule hiyo ambayo awali ilikuwa ikimilikiwa na Mufindi Education Trust (MET) ilikuwa na changamoto ya uendeshaji na Sasa Halmashauri ilikaa na kuomba kuinunua ili kupunguza kadhia ya shule .
0 Comments