Header Ads Widget

HUYU NDIO WAKILI ONESMO OLENGURUMWA TOKA KIJIJI CHA SAKALA OGOSOROCK NGORONGORO


#Uchambuzi wa Wasifu wa Onesmo Kasale Olengurumwa

 

Makala ya Paul Dudui, 

Loliondo

 

Utangulizi

Makala hii inamchambua kwa ufupi, Wakili Msomi Onesmo Olengurumwa, uchambuzi huu unakuja kutokana na kutajwa mara kwa mara nyakati za Uchaguzi katika Jimbo Ngorongoro, hata hivyo mwandishi wa Makala hii anataharisha kwamba uchambuzi huu haumaanishi kwamba  Onesmo Olengurumwa Kasale anatia ya kugombea Ubunge bali ni kutokana na kariba ya Wana Ngorongoro kumtaja mara kwa mara bila yeye mwenyewe kujitokeza kugombea . 


1. KUZALIWA

Onesmo Kasale Olengurumwa ni wakili msomi,ambapo alizaliwa mwaka 1980, katika kijiji cha Sakala, Kata ya Ogosorock, Loliondo, Wilayani Ngorongoro.


2. ELIMU

Onesmo alisoma katika Shule msingi sakala, na badaye alisoma masomo ya Sekondari katika shule ya Sekondari ya Arusha Catholic Seminary kwa kidato cha kwanza hadi cha 4 "O Level". Onesmo aliendelea na Elimu ya A level katika Shule ya Sekondari ya  Dakawa Morogoro ambapo alisoma kidato cha 5 na 6 mwaka 2004 


Onesmo Kasale Olengurumwa, ana digrii 2, ambapo ya kwanza ni digrii ya sheria toka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na digrii ya pili ya uzamivu katika maswala ya utafiti na sera za umma (Masters in Research and Public Policy) chuo kikuu cha Dar es Salaam. 


Onesmo, kitaaluma ni wakili wa Mahakama kuu Tanzania baada ya kuhitimu katika Chuo cha mafunzo kwa Vitendo kwa wanasheria (Law School of Tanzania). Lakini pia amesoma kozi mbalimbali za haki za binadamu, sheria na utawala ndani na nje ya Tanzania. 

 

3. FAMILIA na MAKAZI

Onesmo, ana familia, mke na watoto, makazi yake kwa sasa yapo Jijini Dar es Salaam na kijijini Sakala Loliondo.  


4. KAZI

Wakili Msomi Onesmo Kasale Olengurumwa, amekuwa akifanya kazi za utetezi wa haki za Binadamu toka akiwa Chuo kikuu ambapo alikuwa Rais wa Chama cha Haki za Binadamu Chuo Kikuu cha Dar es Salaam


Onesmo Olengurumwa  aliwahi kufanya kazi katika Kituo cha Sheria na haki za Binadamu (LHRC) Kati ya mwaka 2010-2012 


Kwa sasa Wakili Msomi Onesmo Olengurumwa ni Mratibu wa Kitaifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC).


5. USHIRIKI KATIKA MASUALA YA KIJAMII

Onesmo Olengurumwa, amekuwa Mtetezi wa muda mrefu wa haki za binadamu hapa Tanzania, ambapo anafahamika sana kwa misimamo yake katika  masuala ya utetezi wa haki za binadamu na sheria. Amezunguka nchi nzima kusikiliza na kutatua changamoto za Watanzania wenye changamoto za haki zao. 


Wakili Onesmo, ameshiriki na kujishughulisha kwa kiasi kikubwa  katika kutetea haki za wanangorongoro hasa masuala migogoro ya ardhi. Amekuwa mstari wa mbele katika kuwaongoza na wakati mwingine kuwasemea wanangorongoro katika migogoro mbalimbali inayowakumba kwa miaka mingi. 


6. SIASA na UONGOZI

Wakili Onesmo Olengurumwa amekuwa mwanachama na kada wa CCM toka 2005 


Mwaka 2008 hadi 2012 alikuwa mjumbe wa Baraza la UVCCM Mkoa wa Arusha, kutokea Wilaya ya Ngorongoro, 


Wakili Onesmo, pia aliwahi kugombea Uwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Ngorongoro.


Wakili Msomi Onesmo Olengurumwa, kwa sasa ni Mkurugenzi wa THRDC


Wakili Msomi Onesmo Olengurumwa, Aliachana shughuli za kisiasa toka Mwaka 2010 na kujikita katika masuala ya utetezi wa haki za binadamu


Wakili Onesmo ni Mkurugenzi THRDC. 


Hakuwahi kugombea nafasi yoyote ya kisiasa baada ya kuacha UVCCM mwaka 2012, Hata hivyo Wakili Onesmo amekuwa karibu sana na siasa za Ngorongoro kama mshauri wakati wa uchaguzi na katika masuala mbalimbali ya kimaendeleo na kijamii. 


Wakili Onesmo, ni mtu anayeipenda sana Wilaya yake ya Ngorongoro na watu wake, ambapo amekuwa msaada katika masuala mbalimbali ya kijamii na watu binafsi wanaopata changamoto za kisheria, ikiwa ni pamoja na kusaidia kwenye kesi mbalimbali.

 

Wakili Onesmo, ni mtu mpenda umoja, na mwenye karba ya kujenga mahusiano watu, na hivyo wachambuzi wa masuala ya kijamii wanaamini Onesmo Olengurumwa akiwa Mbunge wa Ngorongoro ataimarisha zaidi mahusiano ya Wana Ngorongoro ikizingatiwa kwamba Ngorongoro ni wilaya yenye siasa za mirengo na makundi. 


Wakili Onesmo Olengurumwa, ana uzoefu mkubwa katika kujenga hoja, kushawishi na amejenga mtandao mkubwa wa wadau ndani na nje ya nchi na serikalini pia. 


Wakili Onesmo Olengurumwa, pia ni mwanaharakati ambaye amepitia changamoto nyingi kutokana na kazi yake ya utetezi wa haki za binadamu, hata hivyo amebakia na misimamo yake ya utetezi wa haki za binadamu 


Wakili Msomi Onesmo Olengurumwa, kwa sasa anaonekana kuwa karibu na serikali ya awamu sita kuwa Rais Samia Suluhu Hassan, ambapo anasema Serikali ya awamu ya 6 inagusa maeneo mengi ya haki za binadamu na hasa hoja walizokuwa wakizipigia kelele kwa muda mrefu. 


Pamoja na kwamba wengi wanatamani akagombee,  inaonekana ni ngumu kwake kugombea nafasi ya ubunge kutokana na ukweli kwamba anaamini zaidi katika kazi utetezi wa haki kuliko siasa, licha ya wanangorongoro kumtaja kila wakati wa uchaguzi, bila yeye kuonekana uwanjani.  

 

Wakili Msomi Onesmo Olengurumwa, ni kiongozi mahiri katika secta ya Asasi za Kiraia na anayefahamika nje na ndani ya nchi kwa kuwa amekuwa kiungo muhimu sana katika ujenzi wa secta ya asasi za kiraia. 


Baadhi ya wachambuzi wa masuala ya Kisiasa Wilayani wanasema endapo Onesmo akagombea ubunge , wanangorongoro watakuwa wamepata kiongozi mzoefu, mahiri, mtu wa mikakati  na mipango, mtatuzi wa migogoro, kiunganishi na mtetezi asieyumbishwa.

 Endapo serikali itaamua kufanya naye kazi kwa ukaribu, basi pande zote mbili (Serikali na Wananchi) zitanufaika kwa kwa kiasi kikubwa hasa katika kumaliza migogoro ya ardhi iliyodumu kwa muda mrefu.   


Wachambuzi wanaendelea kubainisha kuwa Onesmo Olengurumwa ni mtu mbunifu na mwenye  uwezo wa kubuni kuanzisha miradi mbalimbali na kuisimamia vyema, hivyo kama atakuwa mbunge anaweza saidia sana Wilaya kwa upade wa miradi mbalimbali ya maendeleo


Wakimuelezea Onesmo Olengurumwa baadhi ya viongozi wa kijamii waliozungumza na mwandishi wamesema, Onesmo anatoka katika ukoo wenye historia ya Uongozi na uasisi wa CCM, ambapo wamesema baba yake alikuwa kiongozi wa Chama kuanzia TANU na Baadae CCM na kiongozi wa jamii ambapo hata sasa, binamu yake ndiye mwenyekiti wa CCM wilaya Ngorongoro.


Akizungumza na Mwandishi Wakili Onesmo Olengurumwa, amesema anafahamu kiu ya wanangorongoro ya kumtaka kugombea nafasi ya Ubunge wa Jimbo la Ngorongoro, hata hivyo bado hajaamua kurudi katika siasa. 


Wakili Msomi Onesmo Olengurumwa anasema yeye anaamini kwamba hata bila Ubunge anaweza kuendelea kuwasaidia wanangorongoro kwa  kushauri namna bora ya kuiongoza jamii ya Ngorongoro, hata hivyo amesema presha ni kubwa na endapo ataamua kugombea atatoa taarifa kwa wanangorongoro mapema sana

 

Huyu ndiye WAKILI MSOMI ONESMO OLENGURUMWA

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS