Header Ads Widget

FAINI YA SHILINGI MILIONI 3 KWA MFANYABIASHARA ASIYEZINGATIA MATUMIZI YA MASHINEZA EFD



Na, Titus Mwombeki-MDTV BUKOBA

Wafanyabiashara biashara Mkoani Kagera wametakiwa kuwa na matumizi sahihi ya ya mashine za kielektroniki -EFD ili kuepuka faini ya shilingi milioni 3 Kwa atakayebainika.


Hayo yameaemwa na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA Alphayo Kidata katika mkutano na wafanyabiashara wakubwa na wa Kati Mkoani Kagera uliofanyika katika ukumbi wa mkoa mkoani humo.


Aidha, amesema kuwa  wafanyabiashara hao wanakumbushwa kulipa kodi kwa hiari wanatakiwa Kwa  kuzingatia mambo makuu muhimu hasa  utunzaji wa kumbukumbu za biashara zao, kwani inasaidia katika ukadiliaji na ukusanyaji wa kodi,  hivyo  kunawawezesha maafisa wa TRA kukadilia kodi stahiki na serikali kupata kodi kwa stahiki bila dhuruma.


" Wafanyabiashara mnatakiwa kuwa na matumizi sahihi ya mashine za kielektroniki (EFD) mshine hizi zina uwezo wa kuandika majina pamoja na  namba ya utambulisho wa mnunuzi wa bidhaa hivyo wasiotumia mashine hizo wamo hatarini ya kupigwa faini ya shilingi milioni 3,kuwekwa jera au vyote kwapamoja " 


Sambamba na ilo,ameongeza kuwa wafanyabiashara wanatakiwa kuzingatia ulipaji wa kodi ya serikali  kwa hiari bila kutumia matumizi ya nguvu, huku wakitengeneza mipango ya kulipa madeni ya nyuma ikiwa ni pamoja na kujiepusha na biashara ya magendo kwani muhusika anapokamatwa Mali zake utaifishwa pamoja na vyombo vinavyotumika kusafirishia bidhaa hizo hivyo kuwahimiza kutumia mipaka rasmi ili kuondokana na kufirisiwa hadi kifungo kwa wahusika.




Amesema kuwa mashine za EFD zinapoharibika mfanyabiashara anatakiwa kutoa taarifa ili kubadilishiwa  mashine nyingine.


Naye Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Charles Mbuge amesisitiza kuwa ulipaji wa kodi ya serikali ni jambo muhimu kwa Kila mfanyabiashara  kwani sheria ya Mamlaka ya kodi Tanzania sura ya 3 namba 399 iliyoanzishwa na TRA inaeleza majukumu ya Mamlaka hiyo ikiwa ni pamoja na kukadilia na  kukusanya mapato ya serikali.





Aidha, Meja Jenerali Charles Mbuge amesisitiza kuwa wafanyabiashara  Mkoani humo kwa wanatakiwa kuendelea kutekeleza sheria ikiwa nipamoja na kuendelea kulipa  kodi kwa hiari na amewaomba kuendelea na uzalendo huo ikiwa ni pamoja na kutumia mifumo ya Tehama katika kutoa huduma ya ukusanyaji wa kodi kwa mifumo hiyo inayorahisisha ulipaji wa kodi.


Pia memuhakikishia Kamishna wa Mamlaka hiyo kuwa uongozi wa Mkoa kwa kushirikiana na ofisi yake itaendelea kusimamia maendeleo ya serikali juu ya ukusanyaji wa kodi huku akitoa pongezi kwa TRA Mkoani Kagera kwa namna wanavyojidhatiti katika kukusanya kodi na kuwahimiza kuzingatia haki za walipa kodi na wakusanya kodi kuzingatia wajibu wao.


kwa upande wake mwenyekiti wa chemba ya wafanyabiashara Mkoani Kagera Radislaus Jerad amekemea vitendo mbalimbali kama vile suala la magendo  na kukiri kuwa ni jambo linalowaathili wafanyabiashara na kupelekea serikali kukosa mapato.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI