Header Ads Widget

APIGWA KWA KUMPOTOSHA RAIS


Mwandishi wetu, Arusha

Viongozi wa Mila ya kimasai maarufu kama Laigwanani  wa tarafa ya Ngorongoro,wilaya ya Ngorongoro Mkoa wa Arusha, wamepinga  kauli za mzee Isack Lekisongo  kudai ndiye kiongozi Mkuu wa jamii ya kimasai huku akidai wamasai wa Ngorongoro wanasehemu za kuhamia.



Wakizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha ,viongozi hao wamesema alichofanya Lekisongo ni upotoshwaji uliolenga kumpotosha Rais kuhusu shida za Wakazi wa Ngorongoro.


Mwenyekiti wa viongozi wa Mila tarafa hiyo,Metui ole Shaudo amesema kauli ya Lekisongo ni mwendelezo ya kauli ya ukiukwaji haki za binaadamu Ngorongoro kudai kuwa Wakazi wa Ngorongoro wanasehemu nyingine ya kwenda.


"Kwanza huyu sio kiongozi Mkuu wa Masai Tanzania ametumika kutoa kauli za kutaka kuvuruga mjadala ambao unaendelea kutafuta  Suluhu ya kudumu Ngorongoro"amesema


Metui amemtaka Lekisongo kuomba radhi lakini pia serikali kupuuza kali zake huku akielezea wapo tayari kuendelea na majadiliano.


Naye James Moringe mkazi wa Ngorongoro alisema kablaya  hifadhi ya Ngorongoro kuanzishwa mwaka 1959 kulikuwa na mkataba Jamii ya kimasai ihame Serengeti na kwenda Ngorongoro na ikitokea changamoto yoyote maslahi ya jamii hiyo ndio yatakuwa ya kwanza.


"Sasa hii kauli kuwa watu wameongezeka na kujipanga kupungua inatoka wapi na kudai tupo tayari kuhama inatoka huu ni upotoshwaji kwani eneo la kilomita za mraba 8292 bado Kuna eneo la Makazi  ya watu "amesema


Mwisho.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI