Ikiwa ni siku moja imepita toka itokee ajali eneo la Izazi Wilaya ya Iringa iliyosababisha vigo vya watu wanne na kujeruhi zaidi ya watano ajali kwa Lori kuliginga basi la Isamilo kutokana na uzembe wa dereva wa lori aliyekuwa aliyepita magari yaliyokuwa mbele bila kuzingatia sheria za usalama barabarani ajali nyingine yatokea Morogoro asubuhi hii chanzo ni lori .
Mapema asubuhi ya leo malori mawili yaliyogongana uso kwa uso eneo la Rombo mkoani Morogoro kwenye barabara kuu ya Iringa -Morogoro yamesababisha barabara hiyo kufungwa .
Mashuhuda wa ajali hii mkoani Morogoro wameieleza Matukio Daima TV kuwa chanzo cha ajali ni uzembe wa mmoja kati ya dereva wa Lori ambae anachangiwa kuendesha lori hilo akiwa amelewa ama kuanzia .
Hata hivyo walisema hakuna kifo katika ajali hiyo zaidi ya majeruhi.
Matukio ya madereva wa malori kusababisha ajali yanazidi kuongezeka na chanzo kikitajwa kuwa ni uzembe hali inayoendelea kusababisha madhara makubwa kwa binadamu na mali .
Hivyo wameshauri jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani kuanza kuchukua hatua kali kwa madereva wa malori wanaokiuka sheria za usalama barabarani .
0 Comments