Na,Jusline Marco:Arusha
Mkuu wa Mkoa wa Arusha CPA. Amos Makalla amesema Mkoa wa Arusha ni Mkoa wa pili katika kuchangia pato la Taifa ukitanguliwa na Mkoa wa Dar es salaam, huku ukiwa ni Mkoa wa kidiplomasia.
CPA. Makalla ameyasema hayo Leo Oktoba 3, 2026 katika hafla ya kuwaapisha wakuu wa Wilaya wapya ambapo amesema mbali na Mkoa wa kuwa katika nafasi ya pili katika uchangiaji wa pato la taifa, pia ni kitovu cha Utalii kupitia Utalii wa michezo, Mkutano, vivutio mbalimbali, utamaduni na matibabu.
"Lazima tufike mahali kama Mkoa kubeba agenda ya kuhifadhi utamaduni katika Mkoa wa Arusha"Alisema CPA Makalla.
Sambamba na hayo CPA Makala amesema ili mambo hayo yaweze kufanyika ni lazima suala la usafi katika maeneo yote ya Wilaya uzingatiwe ambapo wataka viongozi hao wapya kusimamia suala hilo.
Vilevile amewataka Wakuu hao wapya walioapishwa kuhakikisha Ofisi za Umma zinakuwa kimbilio la wananchi kwa kusikiliza na kushughulikia kero zao kwa wakati, huku akisema hatua hiyo ni sehemu ya utekelezajiwa ahadi ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuacha tabasamu kwa wananchi.
Mhe. Makalla amesema wananchi wanapofika katika Ofisi za Serikali wanapaswa kuona kuwa kero zao zimepokelewa, kusikilizwa na kuchukuliwa hatua, akisisitiza kuwa viongozi hawapaswi kulea migogoro wala madukuduku ya wananchi.
Akiwapongeza Wakuu hao wa Wilaya, Mhe. Makalla pia amesema Mkoa wa Arusha una nafasi muhimu kiuchumi, kidiplomasia na katika sekta ya utalii, hivyo amewataka kusimamia kwa ufanisi maeneo hayo, ikiwemo kuhakikisha malango ya Mkoa yanakuwa safi na kuvutia wageni na watalii wanaofika Mkoani hapa kupitia Uwanja wa ndege wa Kilimanjaro KIA na wale wanaotoka kupitia Wilayani Arumeru.
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini Paulo Makonda amewataka viongozi hao kuendelea kusimamia miradi inayoendelea kutekeleza iweze kukamilika kwa wakati.









0 Comments