Header Ads Widget

NAIBU MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI SAMWEL MANENO AFUNGUA RASMI MAFUNZO MAALUM YA MABADILIKO YA UTAMADUNI WA KAZI


Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe. Samwel M. Maneno amefungua rasmi mafunzo maalum ya Mabadiliko ya Utamaduni wa Kazi (Culture Change) kwa Watumishi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, akisisitiza umuhimu wa kuleta mageuzi ya kifikra ili kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma za kisheria nchini

Mafunzo hayo yanafanyika kwa siku 2 kuanzia tarehe 26 hadi 27 Februari, 2026 Jijinii Dodoma.

Katika hotuba yake ya ufunguzi,  Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali amebainisha kuwa mabadiliko hayo ni sehemu ya mkakati wa serikali wa kuboresha utendaji kazi na kuendana na kasi ya mabadiliko ya kiteknolojia na kijamii.

Aidha, Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, ameeleza kuwa Watumishi wametakiwa kuzingatia maadili ya kazi na kutoa ushauri wa kisheria wenye tija na kwa weledi ili kulinda maslahi ya Taifa.

*"Mabadiliko ya kweli hayaanzi na mifumo pekee, bali yanaanza na fikra za kila mmoja wetu. Tunataka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu iwe kioo cha ufanisi na nidhamu katika utumishi wa umma."* Amesema Mhe. Maneno

Vile vile, Mhe. Maneno amesisitiza umuhimu wa Watumishi kuielewa  na kuifuata Dira ya Taifa 2050, kwani mipango ya maendeleo ya Taifa imejikita katika Dira hiyo.

*“Dira 2050, imetambua nguvu kazi yenye ujuzi na ari kufanikisha lengo la kuufikia uchumi jumuishi wa ngazi ya juu hili ni lengo la Taifa”* amesema Mhe. Maneno

Awali, akimkaribisha Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Bi. Mariam Mangare akimuwalisha Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu, amesema mafunzo haya ni muhimu na yatasaidia watumishi kujenga maadali , kufata sheria na miongozo iliyowekwa na kuongeza ushirikiano wa mawasiliano.

Mafunzo ya culture change kwa Watumishi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali  yanalenga kujenga mazingira ya kazi yanayohimiza ushirikiano, ubunifu, na kuheshimiana miongoni mwa watumishi wa ngazi zote.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI