Header Ads Widget

UBIA WA DP WORLD NA ADANI GROUP WAKUZA PATO LA TAIFA NA UFANISI BANDARINI


Msemaji Mkuu wa Serikali Bw. Gerson Msigwa amesema uwekezaji katika bandari ya Dar Es Salaam kati ya Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) na wabia wa Kimataifa DP World na Adani Group umeleta mapinduzi makubwa ya kiuchumi nchini, ikiwa ni pamoja na kuongeza uwezo wa shehena zinazohudumiwa Bandarini hapo kutokana na kuongezeka kwa ufanisi na kuaminika kwa bandari hiyo.

Msigwa amebainisha hayo leo Jumanne Januari 20, 2026 wakati wa Mkutano wake na Waandishi wa habari mara baada ya kutembelea Bandari hiyo na kuangazia uwekezaji uliofanywa chini ya serikali ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

"Shehena zinazohudumiwa kwenye Bandari yetu ya Dar Es Salaam zimefikia tani Milioni 27. 7 kwa mwaka 2024/25 sawa na ongezeko la asilimia 17 kulinganisha na mwaka uliopita. Muda wa meli kuhudumiwa umepungua pia kutoka siku 30 au wakati mwingine 46 hadi kufikia siku 6." Amesema Msigwa.

Aidha katika mwaka huu, Msemaji huyo wa serikali amebainisha kuwa kuanzia Julai hadi Disemba 2025, tayari Bandari ya Dar Es Salaam imehudumia shehena ya mizigo ya Tani Milioni 16.7 sawa na ongezeko la asilimia 30 kulinganisha na kipindi kama hicho kwa mwaka ulioisha, akisema matarajio kwasasa ni kuwa na mapinduzi makubwa ya kufikia tani Milioni 32 za shehena.

Aidha Serikali pia imesema hadi Juni mwaka 2025, jumla ya wafanyakazi 764 wamepata ajira za moja kwa moja katika fani mbalimbali bandarini hapo, ikiwemo Makarani na waendesha mitambo sambamba na ajira nyingine nyingi zisizokuwa za moja kwa moja kwa Vijana wa Kitanzania.



 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI