Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amejumuika pamoja na Viongozi mbalimbali na Wananchi katika Taarab Maalum iliyoandaliwa katika kuadhimisha Miaka 62 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Taarab hiyo Maalum, iliyopigwa na Kikundi cha Taifa cha Taarab, imefanyika tarehe 12 Januari, 2026 katika Hoteli ya Golden Tulip, Uwanja wa Ndege, Mkoa wa Mjini Magharibi, ikiwa ni kilele cha Maadhimisho ya Miaka 62 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Katika usiku huo wa burudani ya kiutamaduni, waimbaji mahiri wa Kikundi cha Taifa cha Taarab waliupamba ukumbi kwa kuimba nyimbo zenye kuenzi historia ya Mapinduzi ya Zanzibar pamoja na nyimbo maalum za kumpongeza Rais Dkt. Hussein Ali Mwinyi kwa juhudi zake za kuwaletea wananchi maendeleo ya kijamii na kiuchumi Zanzibar .






















0 Comments