Na Hamida Ramadhan, Matukio Daima Media Dodoma
CHAMA Cha Mapinduzi CCM kimeonya vikali dhidi ya kauli na mienendo inayopotosha ukweli kuchafua historia ya Taifa na kuhujumu amani kwa maslahi binafsi kikisisitiza kuwa hakitaruhusu siasa za jazba chuki na migawanyiko.
Onyo hilo limetolewa Leo Januari 17 ,2026 na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa NEC Itikadi Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa Kenani Kihongosi wakati akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dodoma.
Kihongosi amesema CCM ni chama kinachojengwa juu ya misingi ya maridhiano umoja na kuheshimiana hivyo hakitovumilia juhudi zozote za kupotosha ukweli au kueneza chuki zisizo na tija kwa Taifa.
Amesema CCM inamheshimu Waziri Mkuu na Jaji Mkuu Mstaafu Joseph Warioba kwa mchango wake mkubwa alioutoa kwa Taifa lakini ikamtaka kuendelea kufurahia maisha ya kustaafu kwa utulivu bila kutoa malalamiko.
"Ni jambo la kawaida kwa viongozi waliotumikia Taifa kuheshimiwa lakini wastaafu wanapaswa kutoa nafasi kwa viongozi waliopo kuendelea na majukumu yao Kihongosi, "amesema
Nakuongeza kuwa "Licha ya Jaji Warioba kukutana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan bado alionekana mitandaoni akitoa kauli zenye malalamiko hali aliyoitaja kuwa haina tija kwa maendeleo ya Taifa, ".
Kuhusu ziara ya kitaifa Kihongosi alisema kuanzia Januari 18 2026 ataanza ziara ya kichama itakayohusisha mikoa yote ya Tanzania kuanzia mkoani Singida Ziara hiyo inalenga kusikiliza na kutatua kero za wananchi kuimarisha chama na kufuatilia utekelezaji wa ahadi za Rais Samia
" Ziara hii ni jukwaa la wananchi kama kuna anayehisi kuonewa au kunyanyaswa tunawakaribisha waje ili tusikilize na kutatua changamoto zao, "Kihongosi
Kihongosi pia ametoa pongezi kwa Rais Samia kwa kukutana na Mabalozi wa Tanzania Januari 15 2026 katika kikao cha ufunguzi wa mwaka akisema mkutano huo umeimarisha hadhi ya Tanzania kimataifa na kuonesha mwelekeo chanya wa diplomasia ya nchi.
Pia ametoa pongezi kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA kwa kuimarisha mifumo ya ukusanyaji wa kodi ambapo makusanyo yamefikia shilingi trilioni 3 1 na mwezi Desemba kuvuka zaidi ya shilingi trilioni nne .
Kuhusu masuala ya kijamii Kihongosi amesema Serikali inaendelea na maandalizi ya uzinduzi wa bima ya afya kwa wote huku ikichukua hatua za kuondoa tabia ya kuzuia maiti kwa wagonjwa wasiolipa gharama za matibabu.
Aidha ameeleza kuwa Serikali imetekeleza ahadi ya ajira kwa kutoa ajira zaidi ya 12 000 katika sekta mbalimbali na mpango wa kutoa shilingi bilioni mbili kwa ajili ya kuwawezesha vijana bado unaendelea








0 Comments