Header Ads Widget

TANAPA YANG'ARA TUZO ZA WAHASIBU NA WAKAGUZI (NBAA)


Na. Edmund Salaho/ Dar es Salaam.


Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) limetangazwa kuwa Mshindi wa Pili wa Tuzo za Uandaaji Bora wa Taarifa za Hesabu kwa kufuata IPSASs– International Public Sector Accounting Standards kipengele cha Taasisi za Umma " Government Agency Category" kwa hesabu za mwaka 2024.

Tuzo hii imetolewa leo 04.12.2025 na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA) katika Hafla iliyo­fanyika katika Hoteli ya APC, Bunju jijini Dar es Salaam

Akipokea tuzo hiyo kwa niaba ya Kamishna wa Uhifadhi TANAPA, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi - Huduma za Shirika, CPA(T) Abdallah Kiwango amesema ushindi huo ni chachu kwa TANAPA katika kuendelea kuboresha utendaji wake katika maeneo ya Hifadhi za Taifa Nchini.


"Ushindi huu ni ishara ya wazi kuwa faida inayopatikana kutokana na usimamizi wa rasilimali za wanyamapori inatunzwa ipaswavyo na inakwenda kutumika kwenye miradi ya maendeleo nchi yetu Tanzania" alisema Kamishna Kiwango.

Si mara ya kwanza kwa TANAPA kuibuka kidedea katika tuzo hizi ambapo mafanikio haya yameendelea kuchochea kuimarika kwa utendaji kazi ndani ya TANAPA.

Tuzo hiyo ya Mshindi wa Pili imekabidhiwa kwa TANAPA na Naibu Waziri wa Fedha Mhe. Laurent Deogratius Luswetula (Mb).






Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI