Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Mshamu Ali Munde amesema Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET) ni sehemu muhimu ya mageuzi ya elimu ya juu nchini.
Mhe. Munde ameyasema hayo Disemba 19, 2025 katika Mahafali ya 27 ya Chuo cha Uhasibu Arusha, yaliyofanyika katika Kampasi ya Arusha.
Mhe. Munde amesema kupitia Mradi wa HEET, IAA imeboresha miundombinu ya kufundishia na kujifunzia , imejenga na kukarabati wa majengo ya kisasa katika Kampasi za Arusha, Babati na Songea na hivyo kuongeza uwezo wa chuo kupokea wanafunzi wengi zaidi.
Mhe. Munde ameongeza kuwa IAA imenunua vifaa vya TEHAMA vya kisasa na kutengeneza madarasa janja (smart glasses) na kutoa mafunzo kwa Wahadhiri ili waweze kufundisha kwa mbinu zinazokidhi viwango vya kimataifa.
Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa Chuo IAA, Dkt. Mwamini Tulli chuo kinaendelea kuboresha na kupanua miundombinu ya kufundishia na kujifunzia ikiwemo madarasa, ofisi za wahadhiri, maktaba na miundombinu ya TEHAMA katika kampasi zake zote za Arusha, Babati, Dar es Salaam, Dodoma na Songea. Vile vile, chuo kinaendelea kujipanga kuwekeza nguvu na rasilimali katika ujenzi wa kampasi mpya ya Bukombe.













0 Comments